Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, September 26, 2012

OKWI KUKOSA MECHI YA YANGA


KAMSHINA MMOJA AONDOLEWA KWENYE LIGI
Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana jana (Septemba 25 mwaka huu) kupitia ripoti za mechi 21 za Ligi Kuu ya Vodacom ambazo zimeshachezwa mpaka sasa, na kuzifanyia uamuzi wa kikanuni ikiwemo kumuondoa Kamishna mmoja.
 
George Komba aliyekuwa Kamishna kwenye mechi namba 20 kati ya Simba na Ruvu Shooting ameondolewa kwenye orodha ya makamishna wa ligi kutokana na upungufu uliojitokeza katika ripoti yake.
 
Klabu ambazo zimeandikwa barua za onyo ni African Lyon kwa kwenda uwanjani na jezi tofauti na zile ilizoonesha kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi (pre match meeting), Mtibwa Sugar kwa kuchelewa kuwasilisha leseni za wachezaji wake wakati wa mechi na Ruvu Shooting kwa ushangiliaji uliopita kiasi kwenye mechi yao dhidi ya Simba.
 
Kamati pia imethibitisha kadi nyekundu ya Emmanuel Okwi kwa kumpiga kiwiko Kessy Mapande wa JKT Ruvu, hivyo kwa mujibu wa Kanuni ya 25(1)() anakosa mechi tatu na kulipa faini ya sh. 500,000. Mchezaji huyo atakosa mechi namba 20, 27 na 80.
 
Kwa upande wa waamuzi, Ronald Swai ameandikiwa barua ya onyo kutokana na upungufu alioonesha kwenye mechi kati ya Simba na Ruvu Shooting iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Wamiliki wa viwanja vya Mkwakwani, Tanga na Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya wameandikiwa barua ya kuvifanyia marekebisho viwanja vyao katika maeneo mbalimbali yenye upungufu ikiwemo uzio wa kutenganisha wachezaji na washabiki.
 
Mchezaji Faustin Lukoo wa Polisi Moro ambaye kwa mujibu wa ripoti ya mwamuzi aliyemtoa nje kwa kadi nyekundu alimtukana mchezaji mwenzake kwenye mechi dhidi ya African Lyon na Katibu wa Oljoro JKT aliyemwaga maji kwenye chumba cha timu ya Polisi Moro, masuala yao ni ya kinidhamu, hivyo yamepelekwa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi kwa ajili ya hatua zaidi.
 
Kwa klabu ambazo timu zao mpaka sasa zinacheza mechi bila kuwa na logo ya mdhamini, suala hilo limepelekwa kwa wadhamini Vodacom kwa vile wenyewe ndiyo wanaogawa vifaa hivyo.

No comments :

Post a Comment