Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, September 21, 2012

TPBC YAIPIGA JEKI BFT




Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) imelipiga jeki Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Nchini (BFT) katika mashindano yaliyomalizika jana katika uwanja wa ndani wa Taifa.


Rais wa TPBC, Onesmo Ngowi (pichani) alimkabidhi Katibu Mkuu wa BFT bwana Makore Mashaga zawadi za washindi wa kwanza na wa pili katika mashindano ya ngumi za ridhaa za taifa yaliyoshirikisha mabondia kutoka katika mikoa zaidi ya 19 ya Tanzania bara.

Ngowi alimweleza Katibu Mkuu wa BFT kuwa TPBC inaungana na BFT katika kuendeleza ngumi nchini wakijua wazi kuwa ni katika mashindano kama haya Tanzania inawapata wawakilishi wake katika mashindano ya kimataifa.

Ushirikiano huu wa TPBC ulianza tangu wakati wa Katibu Mkuu wa zamani wa iliyokuwa TABA marehemu Narcis Tarimo.

Akimwelezea zaidi msaada wa TPBC katika mashindano ya taifa, Rais wa TPBC bwana Onesmo Ngowi alisema kuwa ni ngumi za ridhaa pekee ambazo zinaweza kuleta mwelekeo wa maendeleo ya ngumi nchini.

Ngowi alisema kuwa kama hakuna msingi mzuri wa ngumi za ridhaa ni wazi kuwa hakutakuwa na ngumi nzuri za kulipwa kwani msingi wa ngumi unaanzia kwenye ngumi za ridhaa.

Rais huyo aliyekuwa bondia maarufu wakati wa ngumi za ridhaa na kulipwa miaka ya 80 na 90 kiasi cha lupewa jina la “Piston Mover”(mwendo wa piston ya gari) kwa ajili ya kasi ya mikono na miguu yake alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kufundisha ufundi kwa mabondia ili waweze kucheza ngumi za ufundi.

“Kuna tofauti kubwa sana kati ya ngumi za ridhaa na ngumi za kulipwa” aliendelea kusisitiza Rais huyo.

“Wakati mabondia wa ridhaa wanapewa points wakati wanapopiga ngumi za ufundi za kichwani, bondia wa ngumi za kulipwa anatakiwa aweze kumzidi mpinzania wake kwa kila kitu” aliendelea kusisitiza Rais huyo.

Mabondia wetu wa ridhaa wanatakiwa wafundishwe namna ya kupiga ngumi za ufundi kichwani na ziwe nyingi ndipo wanaweza kushinda kwenye mashindano ya kimataifa” alimalizia kusisitiza Ngowi.

Ushirikiano wa TPBC na BFT unaleta sura mpya kwenye tasnia ya ngumi nchini na inaonyesha mwanga mzuri mbele ta safari.
Imetolewa na Uongozi

Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC)

No comments :

Post a Comment