Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, September 12, 2012

Mkutano wa 58 wa Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) wafunguliwa rasmi Mjini Colombo, Sri Lanka ,Spika Wa Bunge Anne Makinda Audhuria



   Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa akihutubia Maspika, Wabunge na maafisa zaidi ya 850 kutoka Mabunge ya nchi wanachama jumuiya ya madoloa wakati wa ufunguzi rasmi wa mkutano huo.
    Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwasili katika ukumbi wa MNelum Pokuna Mahinda Rajapaksa kuhudhuria ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 58 wa chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) uliofunguliwa leo na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa.  Aliye pembeni yake ni Mjumbe wa CPA Tawi la Tanzania na Mbunge wa Kigoma Mhe. Zitto Kabwe.
 Spika wa Bunge. Mhe. Anne Makinda akifuatilia kwa umakini ratiba ya ufunguzi wa Mkutano wa 58 wa chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) kabla ya ufunguzi rasmi leo Mjini Colombo Sri, Lanka, aliye kushoto kwake ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pande Ameir Kificho na Mhe. Zitto Kabwe na aliye kulia ni Mhe. Mussa Azzan Zungu. Mkutano huo umefunguliwa rasmi leo na Rais wa Nchi hiyo Mhe. Mahinda Rajapaksa
 Spika wa Bunge. Mhe. Anne Makinda akiteta jambo na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pande Ameir Kificho pamoja na Mhe. Zitto Kabwe wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 58 wa Chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) leo Mjini Colombo, Sri Lanka. Mkutano huo umefunguliwa rasmi na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa. Wa Kwanza kulia ni Afisa dawati wa CPA tawi la Tanzania Ndg. Said Yakubu
  Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akishangaa jambo wakati wakiwa katika mazungumzo na Spika wa Kenya Mhe. Kenneth Marende mara baada ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 58 wa CPA unaofanyika nchini Sri Lanka
 Mhe. Zitto Kabwe akiteta jambo na Mbunge toka Uganda (hakufahamika jina mara moja) pamoja na Spika wa Bunge la Malawi Mhe. Henry Chimundu Banda (katikati) mara baada ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 58 wa CPA unaofanyika nchini Sri Lanka. Kulia ni Mhe. Hamad Rashid Mjumbe wa CPA tawi la Tanzania
Wajumbe wote wa Mkutano wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi rasmi leo.Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge

No comments :

Post a Comment