****************************
Airtel
yakabishi hundi ya shilling million 40 kwa Kitengo cha Usalama
Barabarani kufanikisha wito wa mwaka huu “Usalama Barabarani unaanza na
mimi wewe na sisi sote”.
Dar Es Salaam , Jumanne, Septemba 17, 2013 kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekabidhi Kitengo cha Usalama Barabarani kiasi cha shilling milioni 40 katika kuhakikisha elimu kuhusu usalama barabarani inatolewa ili kuthibiti idadi ya ajali za barabarani nchini.
Hundi hiyo imekabidhiwa na meneja mawasiliano wa Airtel Jackson Mmbando kwa mkuu wa wa Kitengo cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu za Usalama Barabarani.
Kutangazwa kwa ushirikiano huo ambapo Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani Tanzania Kamanda Mohamed Mpinga ametangaza wiki ya nenda kwa usalama barabarani ya mwaka huu itakayozinduliwa rasmi siku chache zijazo huko mkoani Mwanza.
Akiongea wakati wa halfa hiyo mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga alisema” nachukua fursa hii kuwashukuru wadhamini wakuu wa kampeni ya usalama barabarani kwa mwaka huu kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, kwa kutoa mchango wao wa pamoja na kushirikiana na jeshi la polisi usalama barabarani kufikia malengo kwa kuhakikisha usalama wa raia na kupunguza ajali za barabarani ”
Ajali za barabarani zinaongezeka kwa kasi na kusababisha upotezaji wa nguvu kazi huku zikiacha maafa makubwa kwa taifa, ni jukumu la kila mtanzania kuwa sehemu ya kusimamia na kuzingatia sheria za barabarini huku tukiishi na kutimiza kauli mbiu ya mwaka huu “Usalama Barabarani unaanza na mimi wewe na sisi sote”.
Nachukua fursa hii kuwaaasa watumiaji wa vyombo vya moto kupeleka magari yao kukaguliwa na kuthibitishwa ubora wa kutembea barabarani ili kuhakikisha vyombo vinavyotumika kubeba abiria viko salama na vinakidhi viwango vilivyowekwa kuhakikisha usalama barabarani.” aliongeza Mpinga
Akiongea kwa niaba ya Airtel, meneja mawasiliano wa Airtel Jackson Mmbando alisema “kwa muda wa miaka mitano sasa Airtel tunajivunia kuwa sehemu ya juhudi za kuokoa maisha ya watanzania na mali zao na tunayo dhamira ya kuhakikisha tunashirikiana na wadau wote wenye wito wa kusaidia usalama barabarani na jeshi la polisi usalama barabarani kupunguza ajali za barabarini kwani moja ya dhamira ya Airtel ni moja kati ya shughuli za kijamii tunazozifanya nchini.
Nia na madhumuni yetu makubwa ni kusaidia shughuli zinazofanywa na jeshi la polisi kusimamia na kupunguza matokeo ya ajali za barabarani, kila mwaka kunakua na matukio ya ajali za barabarani ambazo zingeweza kuepukika kama wahusika wangekua na elimu ya kutosha. Hii ndio sababu kubwa na madhumini ya Airtel kuwa mmoja wa washiriki wakuu katika kusaidia kuhamasisha na kutoa elimu itakayofanikisha upungufu wa ajali barabarani kwa muda wa miaka mitano sasa.”.
Airtel kwa mwaka huu imechangia kuchapisha stika, kutoa elimu kwa kwa waendesha Boda Boda, ashindano ya mpira kuhamasisha vijana pamoja na kutoa vitu mbalimbali ikiwemo T shirt 500 zenye ujumbe wa mwaka huu “Usalama Barabarani unaanza na mimi wewe na sisi sote”.
Tunaamini ajali za barabarani zinaweza kuepukika ikiwa kila moja atafanya sehemu yake Mmbando aliongeza.

No comments :
Post a Comment