Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) (watano kutoka
kushoto msitari wa mbele) akiwa anandamana pamoja na waandamanaji
wanaopinga ujangili wa tembo ‘Tembea kwa ajili ya Tembo’ mara baada ya
kuwapokea leo, Ubungo jijini Dar es Salaam asubuhi. Maandamano hayo
yamechukua muda wa siku 19 na waandamanaji wametembea kilomita 650,
kutoka Jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof. Alexander Songorwa (aliyeshika karatasi nyeupe mstari wa mbele) akiwa ameungana
na msafara wa waandamanaji eneo la Ubungo kutembea nao hadi viwanja vya
Mnazi Mmoja ambapo atapokea risala kutoka kwa waandamanaji.
Matembezi hayo ya kupinga ujangili yameandaliwa Bw. Patric Patel, Mkurugenzi, African Wildlife Trust (wanne kutoka kulia msitari wa mbele)
yakiwa na lengo la kuelimisha wananchi na Ulimwengu mzima kwa ujumla
juu ya madhara ya ujangili. Matembezi yamehusisha raia wa nchi
mbalimbali duniani.
Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) ambaye ndiye mgeni rasmi katika kilele cha matembezi hayo ametoa wito
kwa wananchi wote waendelee kushirikiana na serikali kupiga vita
ujangili kwa kuwafichua majangili popote wanapowaona; na taasisi zote za
umma zishirikiane kupambana na ujangili ili kuutokomeza kabisa.
No comments :
Post a Comment