Kikosi cha Mapacha Watatu Band FC
Kikosi cha Mashujaa Band FC
MECHI
iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa kati ya Mapacha Watatu FC na
Mashujaa Band FC imeisha vizuri huku timu zote mbili zikifungana bao
1-1, katika mchezo uliochezwa jana katika Viwanja vya Leaders Club,
Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Mchezo
huo uliondaliwa na kundi la Bongo Dansi linalopatikana kataika mtandao
wa kijamii wa facebook kwa nia ya kuletaa ushirikiano na undugu kwa
wanamuziki.
Ilikuwa ni mechi ya kukata na shoka iliyoacha simulizi kubwa kwa wote walioishuhudia. Hadi Mapumziko, Mapacha Watatu walikuwa mbele kwa kwa bao lililofungwa na Hija Ugando dakika ya 19.
Mfungaji
alifunga kufuatia kazi kubwa iliyofanywa na Hamis Dacota aliyeichambua
ngome ya Mashujaa kabla ya kutoa pande kwa mchezaji mwalikwa Mathew
Kiongozi ambaye naye bila hiyana alimsogezea Hajji aliyeujaza mpira
wavuni.
Wachezaji
wa Mapacha wakiongozwa na Jose Mara, Khalid Chokoraa, Kasongo, Dacota ,
Dulla Ngoma na wengineo, waliendelea kulisakama lango la Mashujaa kwa
muda wote wa kipindi cha kwanza.
Lakini
Upepo ulibadilika kipindi cha pili ambapo Chaz Baba, Abdul Tall, Jado
FFU na wengineo walianza kuumiliki mpira na na kuwafunika Mapacha
Watatu.
Zikiwa zimesalia dakika 3 mpira
kumalizika, Mashujaa walisawazisha kwa bao lililofungwa na Hamis Tanya,
ikiwa ni hatua nzuri ya maendeleo ya kundi hilo la Bongo Dansi,
lililoanzishwa na kuongozwa na wadau wa muziki, akiwamo Said Mdoe,
Mathew Kawogo ama Mathew Kiongozi, Engi Muro Mwanamachame, William
Kaijage na Abdulfareed Hussein, Deo Mutta Mwanatanga na Khamis Dacota.
No comments :
Post a Comment