Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, September 5, 2013

SERIKALI YAGAWA PIKIPIKI KWA MAAFISA TARAFA



 Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally N.Rufunga akizungumza na Maafisa Tarafa wa Mkoa wa Shinyanga kabla hajawakabidhi pikipiki zao jana ofisini kwake ( ofisi ya Mkuu wa Mkoa)
 Baadhi ya Maafisa Tarafa wa Mkoa wa Shinyanga wakimsikiliza Mhe.Mkuu wa Mkoa kabla hawajakabidhiwa pikipiki.
 Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Dkt.Anselm Tarimo akitoa maelekezo ya utendaji kazi kwa Maafisa  Tarafa Mkoani Shinyanga.
Baadhi ya pikipiki walizokabidhiwa Maafisa tarafa  Mkoani Shinyanga ili ziwasaidie katika katika utendaji wa kazi zao za serikali.

SHINYANGA, Tanzania

SSerikali mkoani Shinyanga imewataka Maafisa Tarafa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya maadili ya utumishi wa umma ili kuiboresha kada hiyo inayoonekana kusahaulika siku hadi siku.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Ally N. Rufunga amewaasa Maafisa Tarafa ofisini kwake jana,kabla ya  kuwakabidhi pikipiki 14 aina ya YAMAHA kwa ajili ya tarafa zote za mkoa wa Shinyanga, ili kuwasaidia kuboresha utendaji wao wa kazi za serikali.

Mhe. Rufunga amewaeleza kuwa,serikali ya mkoa wa Shinyanga imeamua kubadili mfumo, na kuanzia sasa itawatumia Maafisa Tarafa kikamilifu kwani wao wanawajibika kwa Serikali kuu na Mamlaka za serikali za mitaa katika shughuli zote kuanzia kusimamia ulinzi na usalama hadi usimamizi wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao.

Amewakumbusha pia kuhusu utaratibu wa kuratibu utendaji kazi za serikali katika shughuli mbalimbali katika tarafa zao, na jukumu la kutunza pikipiki hizo.

Nae Katibu Tawala Mkoa Dkt. Anselm Tarimo amewakumbusha Maafisa Tarafa hao wajibu na maadili ya kazi yao na kuwaeleza kuwa wanatarajiwa sana na serikali katika kupata taarifa sahihi za utekelezaji wa shughuli mbalimbali kwenye tarafa, ili serikali iongeze nguvu pale ambapo wenyewe watakwama.

Awali, Maafisa tarafa walieleza changamoto zinazowakabili ni pamoja na kutoshirikishwa katika shughuli za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, hata kutoitwa kwenye vikao vya kisheria na hivyo inakuwa vigumu kwao kuwajibika kwenye shughuli hizo, ambapo uongozi wa Mkoa umeahidi kuzifanyia kazi changamoto hizo kwa kukutana na Wakurugenzi wa Halmashauri zote, ili sheria na kanuni zilizowekwa zifuatwe.

Na Magdalena Nkulu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Shinyanga

No comments :

Post a Comment