Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, September 19, 2013

Mwenge wa Uhuru wawasili Wilayani Masasi,Mkoani Mtwara





Mkuu wa wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Bi Farida Mgomi akisoma taarifa ya wilaya baada ya kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru toka wilaya ya Newala makabidhiano yaliyofanyika katika kijiji cha Ndanda
Msafara wa Mwenge ukikagua kitalu cha miti katika shule
ya sekondari Ndanda.
Mdau Abdulaziz Video kama kawa akiwa mzigoni.
msanii nae akifanya vitu vyake.
Na Abdulaziz Video,Masasi

Katika harakati za kuboresha kiwango cha Elimu wilayani Masasi Mkoani
Mtwara,Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Juma Ali Simai amezindua
Chumba cha masomo ya komputa katika shule ya sekondari ya Ndanda
ambalo limegharimu kiasi cha shilingi milioni 49 zilizotolewa na
wahisani mbalimbali ikiwemo mamlaka ya mawasiliano nchini(TCRA).

Uzinduzi huo uliofanyika katika mbio hizo utawezesha wanafunzi kupata
elimu ya kompyuta na tehama ili kuwajengea uwezo wanafunzi hao
kutokana na upungufu mkubwa wa Vitabu kufuatia kompyuta hizo kufungwa pamoja na huduma ya Intanet.

Akizungumza wakati akizindua jengo hilo la komputa Juma Simai
aliwataka wanafunzi kutumia kompyuta hizo kwa ajili ya kujifunza
zaidi ili kupata elimu juu ya masomo na si kwa kuangalia mambo ambayo
hayatasaidia katika maisha yao ikiwemo utandawazi unaoendelea Duniani
ikiwa pamoja na mambo ambayo hayafuati maadili ya Elimu.

Awali akipokea Mwenge wa Uhuru toka wilaya ya Newala,Mkuu wa wilaya ya Masasi,Bi Farida Mgomi alibainisha kuwa pamoja na wilaya hiyo
kukimbiza Mwenge huo kwa kilometa 120. Miradi itakayotembelewa na kuzinduliwa kabla ya kuukabidhi katika wilaya ya Nanyumbu.

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi walioongea na globu hii walieleza
kuwa uzinduzi wa Chumba cha komputa utasaidia kwa kiasi kikubwa
kuboresha elimu yao.

Mwenge ukiwa wilayani Masasi umetembelea, jumla ya miradi 10 kati ya
miradi hiyo imefunguliwa,kuwekewa mawe ya msingi na kutembelewa yote
ikiwa na thamani ya shilingi Bilioni 2.4 ikiwemo chumba cha kompyuta
kwenye shule ya sekondari ya Ndanda,mradi wa umwagiliaji maji wa
Mpowora,upandaji wa miti ya mbao katika kijij Mwenge i cha Mwenda,ujenzi wa mahabara ya kisasa kwenye kituo cha afya cha Chiwale na kutembelea vikundi vya wajasilia mali, Pamoja na shamra hizo za mwenge pia kulipambwa na burdani ya Bendi ya Vijana Jazz ya Dar es sallam

No comments :

Post a Comment