Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, September 5, 2013

KINANA, NAPE KUUNGURUMA SHINYANGA, SIMIYU, MARA





Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu maandalizi ya zira ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara. (PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

NA MWANDISHI WETU
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Abdulrahaman Kinana, wiki ijayo ataanza ziara ya kikazi katika mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi Nape Nnauye, alisema, ziara hiyo ambayo naye atakuwemo, itaanzia katika mkoa wa Shinyanga Septemba 10 hadi 13 mwaka huu, kwa kutembelea wilaya zote nne za mkoa huo na kufuatiwa na mkoa mpya wa Simiyu kuanzia Septemba 14 hadi 19, pia kwa kutembelea wilaya zote tano.

Nape alisema, Kinana atahitimisha ziara hiyo katika mkoa wa Mara ambako atatembelea katika wilaya sita za mkoa huo kuanzia Septemba 20 hadi 25, mwaka huu.

Alisema pamoja na kuwa ziara hiyo ya kikazi ni ya kawaida, lakini lengo kuu ni kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama, kukagua na kuimarisha uhai wa chama na  kuhamasisha wananchi wa maeneo hayo ambayo kwa kiasi kikubwa ni ya wafugaji, kujituma katika shughuli za uzalishaji ili Kuleta tija katika maisha yao na ya taifa kwa ujumla.

"Katika ziara hiyo Katibu Mkuu, takagua maendeleo ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/2015 hasa katika miradi ya kimaendeleo Kama vile Ujenzi wa majosho kwa ajili ya wafugaji, maendeleo ya maboresho ya kilimo cha Pamba, uvuvi wenye tija pamoja na maboresho ya sekta za Afya, elimu na miundombinu zikiwemo Barabara", alisema Nape.

Alisema, pia katika ziara hiyo Katibu Mkuu  atapata fursa ya kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kwa kushauriana na serikali kutafuta namna ya kuzitafutia ufumbuzi.Katibu mkuu pia atafanya mikutano ya ndani, na ya hadhara katika kila wilaya za mikoa hiyo.

No comments :

Post a Comment