NDUGU ZANGU
WATANZANIA
NDUGU ZANGU WANA
HANDENI
NDUGU MDAU WA
UTAMADUNI, MABIBI NA MABWANA
SALAAM!
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, pichani.
Kwa
heshima kubwa kwako naomba niwasilishe ombi kwenu kwa mdau yoyote wa utamaduni
na Mtanzania kwa ujumla juu ya kuandaa Tamasha la Utamaduni wilaya ya Handeni,
mkoani Tanga, ifikapo Desemba 14 mwaka huu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya Handeni, Dr Khalfany Haule, pichani.
Tamasha
hilo tunakusudia kufanya katika Uwanja wa Azimio. Hata hivyo, Uwanja huu wa
Azimio upo kwenye matengenezo, hivyo tunaweza kuendelea na tamasha letu kwa upande
usiokuwa kwenye ukarabati.
Mbunge wa Handeni, Dr Abdallah Omari Kigoda, pichani.
Ndugu mdau
na serikali kwa ujumla; kwa muda mrefu sasa kumekuwa kukifanyika matamasha ya
kila aina katika mikoa mbalimbali ya Tanzania. Kabla ya yote, napenda
kuwapongeza waandaaji wote wanaoandaa matamasha hayo yenye kujenga jamii
inayoheshimu utamaduni wao
Kambi Mbwana, mratibu wa Tamasha la Utamaduni wilayani Handeni, mkoani Tanga, litakalofanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Yapo
matamasha mengi yanayofanyika katika mikoa hiyo na nisingependa kuorodhesha
yote zaidi ya kuwashukuru na kutambua mchango wao katika sekta ya Utamaduni
hapa Tanzania.
Kwa
kuandaa matamasha hayo na kufanyika kwa mafanikio licha ya kuwa na changamoto
za kiubinadamu, imesababisha kujenga usawa kwa wadau wa utamaduni na wananchi
kwa ujumla.
Leo hii
pamoja namambo mengine, lakini mtu anajiona yupo mtupu, pindi anapodharau utamaduni
wao na kukimbilia tamaduni za watu wan je, hususan waliokuwa kweny Mataifa
makubwa.
Ndugu
zangu wadau wa Handeni Kwetu, wilaya ya Handeni ni kati ya zile zinazokabiriwa
na changamoto nyingi mno. Wilaya hii iliyopakana na wilaya Korogwe, imekuwa
kwenye joto kubwa la kupokea wageni mbalimbali, huku kila mmoja akiwa na
utamaduni wake.
Katika
tamaduni hizo, wapo wale wanaoeneza mambo mazuri na wale wanaoeneza sumu, yani
tamaduni zisizokuwa nzuri nao pia hawakosekani katika utitiri huo.
Kwa wale wanaofahamu
mwingiliano wa watu katika wilaya ya Handeni, watakubaliana na mimi kuwa kuna
kubadilishana kwa tamaduni kutoka upande mmoja kwenda mwingine.
Kwakuwa
lengo ni kuongeza ufanisi katika kujieletea maendeleo yao; hakuna tatizo katika
hilo. Hata hivyo, kwa kulijua hilo, ndipo tulipokaa na kubuni wazo la kuanzisha
Tamasha la Utamaduni la Handeni Kwetu.
Wazo na
jina la Tamasha hili kwa kiasi kikubwa linatokana na kuwapo kwa Mtandao blog
yenye jina la Handeni Kwetu. Blog hii licha ya kupewa jina hilo, lakini
inachanganya habari zote bila kubagua.
Ndio
Gazeti tando lililojipatia umaarufu kwa kiasi kikubwa na kwa haraka mno. Mbali
na blog hiyo, pia kuna forum yenye jina la Handeni Kwetu. Group hili
lilianzishwa maalum kwa ajili ya kupeana mawazo na changamoto za kimaisha
miongoni mwa jamii.
Group hili lilikuwa
na dhamira pia ya kukusanya mawazo mapya na kuunganisha nguvu kwa ajili ya
harakati za kimaisha. Tunashukuru kwa wale waliotuelewa na kushirikiana na
sisi.
Kwa wale
wanaofuatilia group hili, watakubaliana na mimi kuwa kwa sasa tumefikia hatua
nzuri zaidi kwakuwa wengi wao wamekubali kushirikiana mawazo yao kwa ajili ya
jambo la kimaendeleo.
Ndugu
zangu wadau wa Handeni Kwetu; Tamasha la Handeni Kwetu linaandaliwa chini ya
Kampuni inayojulikana kama Raha Company And Entertainment, yenye maskani yake
jijini Dar es Salaam.
Kwa
kupitia Kampuni hii; tunaamini kwa pamoja tutaweza kufanikisha kwa tamasha hili
katika ardhi ya wilaya ya Handeni, mkoani Tanga. Sisi tunaamini kuwa changamoto
nyingi zinaweza kujitokeza, ila tutakabiriana nazo kwa ajili ya kufungua
historia mpya.
Tangu
nchi hii ilipopata uhuru wake, katika wilaya ya Handeni na Tanga kama mkoa
hakujakuwa na fursa kama hizo. Vijana wengi wana vipaji au wanapenda kushiriki
kwenye mambo ya utamaduni, ila wanakosa sehemu ya kuonyesha kwa vjtendo.
Mbali na
hilo, kwa wale wanaotamani kujiingiza kwenye mambo ya utamaduni na sanaa kwa
ujumla, wanakosa sehemu ya kuongeza chachu yao kutokana na uhaba wa matasha ya
aina hii.
Watu
wanajiuliza, hata kama kuna kikundi au mtu anapenda mambo ya utamaduni, ila
wapi aende kuonyesha? Swali jingine ni namna gani anaweza kuishi wakati wote
anapokuwa kwenye harakati hizo?
Maswali
haya na mengine yote yanaongeza ugumu katika kupambana na changamoto za
kimaisha na sekta nzima ya Utamaduni. Pamoja na hayo; ndipo tulipoamua
kuanzisha wazo hili.
Ndugu
wadau wa Handeni Kwetu; Wazo aina hii halijakuja tu kiholela bali liliandaliwa
na kupangiwa mtitiriko wote. Hata kuanzishwa kwa blog au group la Handeni Kwetu
kulikwenda sambamba.
Ni kwa
kupitia blog na group letu, tumeweza kujiingiza katika mtandao mpana wa kuweza
kuuza mawazo yetu. Kuwaonyesha watu kile tunachokijua na kukithamini mbele ya
jamii inayotuzunguuka.
Watu
wanaoishi ndani ya Tanzania na nje ya nchi wamepata sehemu ya kuijua vyema
wilaya ya Handeni. Sisi tunaamini kuwa hata kama sio leo au kesho, ila wapo
wafanyabiashara, wawekezaji wanaweza kuguswa katika kuitembelea wilaya yetu na
kuweka makazi.
Ndugu
zangu wadau wa Handeni Kwetu; kwakuwa tayari tumeamua kuanzisha wazo kama hili,
ni wakati wako wewe unayeguswa na mambo ya utamaduni kushirikiana na sisi.
Tunakuomba
sana, kwa nafasi yako, uweze kushirikiana na sisi katika kufanikisha tamasha
hili la Utamaduni la wilaya ya Handeni. Sisi tunaamini ushirikiano ndio
unaoweza kufanikisha yote hayo.
Msaada
wowote unaoona unafaa tupo tayari kuupokea. Kama unaona una taasisi yako,
Kampuni yako au shirika na kuna uwezekano wa kudhamini, basi unakaribishwa,
ambapo pia ni nafasi ya kujitangaza kwa wilaya hii.
Nashukuru
kwa wale waliokubali kukaa pamoja na kulijadili suala hili hadi kutamani
kudhamini katika Tamasha hili litakalofanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Maandalizi
ya tamasha hili yanaendelea. Mazungumzo mengi yameshafanyika. Hadi kufikisha
wazo hili kwenu, tulikaa chini na kujitafakari kwa kina juu ya kufanikisha kwa
vitendo suala hili.
Ndugu
zangu wadau wa Handeni Kwetu; sisi tunaamini serikali pekee haiwezi kuleta
maendeleo ya mtu mmoja mmoja bila hata kushirikiana. Kwa kufanyika kwa tamasha
hili, tunajua tutafungua fursa nyingine za kimaendeleo wakati wowote kuanzia
sasa.
Tutaweza
pia kukutana kwa pamoja watu wote katika tamasha hilo na kuweza kujadiliana juu
ya mustakabari wa maisha yetu. Tutaweza kuitangaza vyema wilaya yetu.
Watu
wenye nafasi zao, uwezo wao watakapoona juhudi hizo, wanaweza kuingia kwa miguu
yote katika uwekezaji wa wilaya hii. Wote tunajua jinsi changamoto za uhaba wa
maji na umeme unavyosumbua.
Kwa
kufanyika kwa tamasha hili, kuna uwezekano mkubwa makampuni yanayotoa huduma wa
umeme wa jua, uchimbaji wa visima na mengineyo kuguswa na kuwahudumia wananchi
wote.
Pia
tunaamini kuwa kwa kufikia hatua ya kuitangaza kama tulivyofanya kwa kuanzisha
blog na forum, basi wageni wenye dhamira wanaweza kutembelea katika wilaya hii
hivyo kukuza pato la Handeni na Tanzania kwa ujumla.
HITIMISHO
Tunajua
wapo wanaoweza kujiuliza kwanini Handeni? Najua pia wapo watakaojiuliza maana
ya Tamasha hili. Najua pia watu hao wanaweza kuingiza fikra nyingine, hasa za
kisiasa.
Lakini
watu hao wanapaswa kujua kuwa hakuna njia ya mkato inayofanywa katika kufanyika
kwa tamasha hili. Ni kutokana na mapenzi ya dhati kwa wilaya hii, mkoa wa Tanga
na Tanzania kwa ujumla.
Haya na
mengine yote, yamesukuma hamu ya kuanzisha kwa tamasha hili ambalo tunaamini ni
la kwanza kuwahi kufanyika kwa historia ya wilaya ya Handeni, mkoani Tanga,
hivyo tutafurahi kama kila mmoja ataona faida ya kushirikiana na sisi ili tufanikishe
maendeleo.
Katika
hilo, tunaomba serikali kwa kupitia Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu,
Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya, Mbunge wa Jimbo la Handeni, Ofisa Utamaduni wa
wilaya na viongozi watuunge mkono bila kinyongo chochote kwa faida ya Handeni
na watu wake.
Kadri ya
mambo yatakavyosonga mbele, tutaendelea kujulishana kwa kupitia njia mbalimbali
na kuwapa watu fursa ya kufuatilia mwelekeo wa Tamasha la Handeni Kwetu.
Pamoja ni
Ushindi.
Tunathubutu, tutaweza
na tutasonga mbele.
Mungu ibariki Handeni
Mungu ibariki Tanzania na watu wake wote.
Kambi Mbwana,
Mratibu.
No comments :
Post a Comment