SERIKALI
imeyafungia kutochapishwa Magazeti ya MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia
27 Septemba,2013 kutokana na mwenendo wa magazeti hayo kuandika habari
na makala za uchochezi na uhasama kwa nia ya kusababisha wananchi
wakose imani kwa vyombo vya dola hivyo kuhatarisha amani na mshikamano
ulipo nchini.
Gazeti
la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa siku kumi na nne(14) kuanzia
27 Septemba,2013.Adhabu hii imetangazwa kwa Tangazo la
Serikali(Government Notice )Namba 333 la tarehe 27 septemba,2013.
Gazeti
la MWANANCHI limepewa adhabu hiyo kutokana na hivi karibuni kuchapisha
habari zenye mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu wa amani,mfano tarehe 17
Julai,2013 katika toleo Namba 4774 ilichapisha habari isemayo “MISHAHARA
MIPYA SERIKALINI 2013” kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa matumizi
ya vyombo vya habari waraka huo ulikuwa wa Siri haukupaswa kuchapishwa
Magazetini.
Aidha,
katika toleo la Jumamosi,tarehe 17 Agosti,2013 lilichapisha habari
yenye kichwa kisemacho “WAISLAM WASALI CHINI YA ULINZI MKALI” habari
hiyo ilikolezwa na picha ya mbwa mkali mwenye hasira.Habari na picha
hiyo ilitoa tafsiri ya kuwa Jeshi la Polisi lilipeleka Mbwa katika
maeneo ya ibada ya waumini wa dini ya kiislam.Jambo ambalo halikuwa la
ukweli.
Jeshi
la Polisi katika doria siku hiyo halikupeleka mbwa katika maeneo ya
Misikiti.Serikali na jeshi la Polisi linaheshimu na kuzingatia maadili
ya dini ya Kiislamu na kwa hiyo Jeshi lake haliwezi kupitisha au
kuingiza mbwa katika maeneo ya ibada.
Hivyo
basi,kwa gazeti hili kuchapisha habari iliyokolezwa na picha ya mbwa ni
uchochezi wa kulichonganisha Jeshi la Polisi na waumini wa dini ya
kiislam mbwa ni najisi hapaswi kuingia katika maeneo ya ibada.
Gazeti
la MTANZANIA limefungiwa kutochapishwa kwa siku tisini(90) kuanzia
tarehe 27 Septemba,2013 kwa kuchapisha habari zenye uchochezi.Gazeti
hili limeonywa mara nyingi lirekebishe mtindo wake wa uandishi wa
kichochezi na lizingatie maadili na Sheria na Kanuni za fani ya
Habari.
Pamoja
na kuonywa gazeti hili halikuonyesha kuzingatia maelekezo ya Msajili wa
Magazeti, mfano ;katika toleo na 7262 la 20 Machi,2013 liliandika
habari yenye kichwa kisemacho “URAIS WA DAMU”,tarehe 12 Juni,2013,toleo
Namba 7344 lilichapisha makala isemayo “MAPINDUZI HAYAEPUKIKI”.
Aidha,
siku ya Jumatano,tarehe 18 Septemba,2013 katika toleo Namba 73414
ukurasa wa mbele lilichapisha Kichwa cha habari kisemacho “SERIKALI
YANUKA DAMU” taarifa hiyo ilikolezwa na picha zilizo unganishwa kwa
ustadi mkubwa kwa kutumia kompyuta kutapakaza rangi nyekundu mithili ya
damu nyingi kumwagika .Katika habari hiyo gazeti hilo limedai bila
uthibitisho kuwa Jeshi la Polisi linahusika na wahanga waliomizwa na
watu wasiojulikana kwa kumwagiwa tindikali na waliyovamiwa na
kujeruhiwa vibaya.
Vile vile gazeti hilo limeishtumu serikali kuwa goigoi katika kushughulikia matukio yenye sura ya kigaidi.
Kwa
ujumla wake habari hiyo ni ya kichochezi ina lengo la kuwafanya
wananchi wavichukie vyombo vya ulinzi na usalama wavione kuwa
haviwasaidii.
Kutokana
na makosa yalitajwa hapo juu serikali imelifungia gazeti la Mtanzania
kutochapishwa kwa muda wa siku tisini(90) kwa Tangazo la Serikali Namba
332(Government Notice No.332) la tarehe 27 septemba,2013,.
Serikali
inawataka wamiliki,wahariri na wanahabari kwa ujumla kuwa
makini,kuzingatia weledi,miiko na madili yataaluma uandishi wa habari.
Serikali
inawataka wamiliki na hasa wahariri kuhakisha kuwa habari
wanazoziandika na vipindi wanavyoviandaa vinazingatia taaluma,kuweka
mbele maslahi ya taifa letu kwa kuwa na uzalendo wa hali ya juu.
Serikali
inavionya vyombo vya habari vinavyoutumia uhuru wa habari bila wajibu
kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali ikiwemo ya kuvifungia .Serikali
haitakubali kuona vyombo vya habari kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani
nchini.
Imetolewa na
MKURUGENZI IDARA YA HABARI
WIZARA YA HABARI,VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
28 SEPTEMBA,2013
No comments :
Post a Comment