BAGAMOYO
Mkazi
wa kijiji cha Magomeni Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani, Khamisi Tanga
(46), ameota matiti katika hali isiyo ya kawaida ikidaiwa
imesababishwa na kutumia dawa za kupunguza makali ya Ukimwi ARV’S.
Akizungumza na waandishi wa habari waliokwenda Wilayani humo kufanya
utafiti kuhusu utekelezaji wa sheria ya Ukimwi na Chama cha Waandishi
wa habari za Ukimwi (AJAT),Khamisi (Pichani) alisema alipatwa na mkasa
huo miaka mitatu iliyopita.
Akisimulia namna alivyoanza kuugua alisema awali aliona matiti yake
yakiongezeka ukubwa kila kukicha lakini hakujua kama lingeweza kuja kuwa
tatizo kubwa kama lilivyo sasa.
Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya ilimbidi kwenda kliniki
anayohudhuriaga kupata dawa na kuwaeleza manesi ambapo walimjibu kuwa
imesababishwa na dawa anazotumia na hivyo kulazimika kukatizwa dozi hiyo
na kupewa aina nyingine.
Hata hivyo Khamisi alisema kwamba pamoja na kubadilishiwa dozi
hajaona kama kuna mabadiliko yoyote aliyoyapata na kuongeza kwamba hivi
karibuni alipewa dawa nyingine ambazo kati ya hizo kuna zile ambazo
zilimsabishia matiti na tayari ameanza kupatwa na maamuvu aliyokuwa
akisikiaga awali wakati matiti yalivyokuwa yanaanza kuota.
Kwa mujibu wa Khamisi ameshahangaika kupata matibabu hadi Hospitali
ya Rufaa ya Muhimbili lakini hadi leo hajapatiwa tiba stahili ya
kumaliza tatizo hilo.
“Jamani Watanzania naomba wanisaidie kwa njia yoyote ile ili
niondekane na hali hii kwani inanidhoofisha sana na kunikosesha raha
hasa mbele ya wanaume wenzangu.
Kwani
hapa navyoongea na nyie waandishi nilipimwa hadi kansa na matiti ndio
kama hivyo mnavyoyaona yanaendelea kukua na huniuma sana hasa wakati
ninapolala,”alisema kaka huyo.
Pia
alitumia fursa hiyo kumuomba Rais Jakaya Kikwete kumsaidia ili arudi
katika hali yake ya uanaume kwa kuwa maisha kwa sasa kwake yamezidi kuwa
magumu kwa kuwa hawezi kufanya kazi yoyote kutokana na hali hiyo.
Kwa
upande wa mtaalam wa magonjwa, Dk. Dina Komakoma,akielezea kuhusu
sababu za kutokewa kwa hali hiyo kwa wagonjwa wenye maambukizi ya VVU ni
jambo la kawaida japo hutofautiana.
Dk.
Komakoma alisema wengine hujikuta wakinenepa au wakikonda sana na hili
la Khamis sio mtu wa kwanza kupatwa na hali hiyo na kuongeza kwamba
inapotokea mgonjwa akapata hali tofauti kama hiyo anapaswa kusitishiwa
dawa. SOURCE MITANDAO
No comments :
Post a Comment