Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Saturday, September 1, 2012

SACCO - Yapatiwa Mkopo Wa Matrekta Na Benki Ya Raslimali-TIB



Matrekta 11  yaliyotolewa mkopo kwa wanachama wa Talanta SACCOS ya tarafa ya Kinyangiri wilaya ya Mkalama Mkoani Singida.
Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, akizungumza na wananchi kisha alikabidhi matrekta makubwa 11 kwa wanachama wa Talanta SACCOS ya tarafa ya Kinyangiri wilaya Mkalama, yaliyotolewa mkopo na Benki ya rasilimali (TIB), kwa gharama ya Sh.Milioni 450.5.
Mwenyekiti wa Talanta SACCOS tarafa ya Kinyangiri Mayasa Salum,akifurahia trekta alilokopeshwa na benki ya rasilimali (TIB), kupitia SACCOS hiyo.


MKUU wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone akikaribishwa na mmoja wa wanachama wa ‘Talanta SACCOS’ katika kijiji cha Iguguno tarafa ya Kinyangiri wilaya ya Mkalama alipoenda kukabidhi matrekta 11 yaliyogharimu Sh. Milioni 450.5.


Na: Elisante John,Singida

Wananchi wametakiwa kujiunga katika vikundi ili kunufaika na mikopo inayotolewa nataasisi za vyombo vya kifedha. Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Kone,alisema hayo wakati wa kukabidhi matrekta makubwa 11 kwa Talanta SACCOS ya tarafa ya Kinyangiri, wilayani Mkalama, yenye thamani ya Sh. Milioni 450.5 kutoka benki ya raslimali (TIB). Dk. Kone alisema kupitia ushirika wakulima na wananchi kwa ujumla watanufaika na mkakati wa kilimo kwanza.Kwa upande wake mwenyekiti wa Talanta SACCOS, Myasa Salum aliishukru benki hiyo ambayo imelenga kumkomboa mkulima wa kawaida kijijini.

No comments :

Post a Comment