Diwani wa kata ya Kipawa Bonnah Kaluwa akifafanua jambo kwenye mkutano huo, kulia ni Mtendaji wa Mtaa Kipawa Said Fundi. |
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo diwani wa kata ya Kipawa, Bonnah Kaluwa, alisema lengo la mradi huo ni kuboresha Mazingira ya elimu ya Msingi na Sekondari kwenye kata yake.
Aidha Kaluwa alifafanua kuwa Uboreshaji huo wa mazingira ya Elimu unafanyika kwenye Shule saba za Msingi na Sekondary za kata hiyo kwa kuwapatia madawati, maji safi na salama, kujenga vyoo na madarasa pamoja na kuwapatia wanafunzi na walimu vifaa vya elimu.
Awamu ya kwanza ya Mradi huo ilizinduliwa Machi 17,2012 ambapo kwenye awamu hiyo kulifanyika kampeni za kuhamasisha wadau kuchangisha pesa na kufanikiwa kukusanya kiasi cha Tsh.155.5Million, ambazo zilitumika kwa kununua madawati 500 ya Shule ya Msingi, 480 Shule za Sekondari na viti 100 vya shule ya awali pamoja na kufanikiwa kuchimba kisima cha maji katika kila shule.
Awamu hii ya pili ya mradi itajihusisha zaidi kwenye ujenzi wa vyoo na madarasa.
No comments :
Post a Comment