Naibu
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na Mkuu wa 
Wilaya ya Kyerwa, Darry Rwegasira katika Hifadhi ya Rabanda-Rumanyika, 
alipoitembelea kuona shughuli za uhifadhi na kudhibiti ujangili nchini. 
(Picha zote na Mpiga Picha Wetu)
Naibu
 waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiangalia nyaya 
mbalimbali zilizokamatwa kutoka kwa majangili wanaovamia hifadhi za 
Burigi na Biharamulo  Rumanyika alipotembelea ili kuona shughuli za 
uhifadhi na kudhibiti ujangili nchini.
DAR ES SALAAM, Tanzania
SERIKALI
 imeshangazwa na hatua ya wageni kuwavamia mbuga mbalimbali na misitu 
nchini kiasi cha kufanya kuongezeka vitendo vya ujangili na kuahidi 
kuchukua hatua kali ili kutokomeza ujangili huo.
Naibu
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema ili kudhibiti 
hali hiyio hatua za haraka zinahitajika kuchukuliwa ikiwamo na 
kuimarisha ulinzi katika hifadhi na mapori mbalimbali  ambayo mengine 
yameanza ktumiwa na waasi.
Akizungumza
 mjini Bariadi baada ya kuwaona askari wa Kijereshi walioko mahabusu kwa
 kutuhumiwa kuua majangili, Nyalandu alisema kuwa askari wakliopo ni 
wachache kiasi cha kufanya majangili wengi kuvamia hifadhi na kuua 
wanyama hususan tembo.
“Kinachosikitisha
 ni kuwa hawa majangili wamebadilika zamani waklikuwa wanawinda kwa 
ajili ya kupata kitoweo lakini sasa wamebadilika na wanavamia kwa silaha
 za kijeshi na kuua wanyama bila woga” alisema.
Nyalandu
 aliahidi kuwa kwa sasa hali hiyo imekuwa kama janaga la kitaifa na 
hivyo kutaka wananchi kubadilika na kkabiliana na majangili ili kulinda 
maliasili kwa ajili ya vizazi vijavyo.
“Tnahitaji
 kuajili vijana wengi kadri inavyowezekana ili kukabiliana na wimbi 
hili, tunahitaji zaidi ya askari 4,000 na kuanzia mwaka huu tumepewa 
kibakli cha kuajili vijana 400 ambao tutawasambaza katiak hifadhi na 
mbuga nyingine.
Alisisitiza
 kuwa kwa sasa askari hao wanalinda zaidi ya kilometa za maraba 169 
wakati zinazotakiwa ni kilometa za mraba 25 na hivyo kutoa mwanya kwa 
majangili kuingina na kutoka bila ya kupatikana.
Nyalandu
 alisema nchi ilitalajiwa kuwa na tembo 400,000 mwaka huu  miaka 50 
iliyopita na kini kutokana na kukithiri vitendo vya ujangili wamebakia 
tembo 110,000 tu  kitu kinachotishia uwepo wa wanyama hao.
No comments :
Post a Comment