Mshambuliaji
wa Simba, Mrisho Ngassa (kulia) akiwatoka mabeki wa African Lyon,
wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom mzunguko wa pili ulioanza leo.
Mchezo huo umechezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo
Simba imeshinda kwa mabao 3-1.
Matokeo mengine ya mechi za leo ni kama ifuatavyo, Azam Fc 3- Kagera Sugar 1, Ruvu Shooting 1- JKT 0, Orjolo 3-Toto African 1, Polisi Moro 1- Mtibwa Sugar 0, Coast Union 3-Mgambo Shooting 1.
Mrisho Ngassa, akiinuliwa na wenzake nyavuni baada ya kutupia bao la pili.
Mwinyi Kazimoto, akizunguka katikati ya Dimba.
Amri Kiemba, akimiliki mpira katikati ya mabeki wa African Lyon.
Mshambuliaji
wa Simba, Mrisho Ngassa (kushoto) akimtoka beki wa African Lyon, Mussa
Mude, wakati wakati wa mchezo wa fungua dimba mzunguko wa pili wa Ligi
Kuu ya Vodacom, iliyoanza leo kati ya timu hizo kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam. Mpaka sasa Simba inaongoza kwa mabao 3-0 ambapo
mabao ya Simba yamefungwa na Ramadhan Chombo Ledondo, katika dakika ya
3, na mabao 2 yakifungwa na Mrisho Ngassa, katika dakika ya 19 na 39.
African Lyon, walikosa penati katika dakika ya 32 iliyopigwa na Shamte
Ally.
Ni
heka heka katika lango la African Lyon. Wakati huo huo huko katika
uwanja wa Chamanzi, Azam Fc inaongoza kwa mabao 2-0 na viwanja vyote
hivi sasa ni kipindi cha pili. picha zaidi tembelea http://sufianimafoto.blogspot.com/
No comments :
Post a Comment