Watoto
wa kitongoji cha Ifumbo Wilaya ya Mvomero wakipeleka maji na chakula
kwa vijana waliokuwa wakichimba kutengeneza barabara kwa kutumia majembe
ya mkono kama walivyokutwa na kamera ya BRYCESON NYEREGETE.
Na Bryceson Mathias, Mvomero
WAKATI
Serikali ya Kata ya Mvomerowilayani humo ikiwa bado inatafakari
kuwasaidia wananchi wa Ifumbo kupata barabara ili wajawazito
wanaojifungulia njia wawahi kufika kwenye zahanati iliyoko kilomita 10,
akina mama 31 waliojifungulia njiani akiwemo aliyejifungulia chini ya
mwembe Selina Jovini, wamemuomba Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya
IPP, Dk. Reginald Mengi awasaidie kero yao.
Hayo yalisemwa
hivi karibuni na akina Mama Wakazi wa Kitongozi cha Ifumbo wilayani
humo, ikiwa ni mara tu baada ya kuwapelekeaa Maji ya Kunywa na Chakula
Vijana na waume waliokuwa wakichimba Barabara kwa majembe ya Mkono ili
kuwanusuru wake zao waondokane na adha hiyo.
Akizungumza na
Mwandishi wa Habari hizi Selina Jovini, ambaye Mwaka Jana alijifungua
mtoto wa kike chini ya mti wa mwembe baada ya kubebwa umbali wa kilomita
10 na watu wakiwemo wazazi wake kufuata zahanati iliyoko Mvomero mjini kutokana na ukosefu wa barabara alisema,
“Tunamsikia tu
Dkt. Mengi kwenye Radio tunazofungua huku kwetu milimani kusiko na
barabara wala TV, kwamba anawasaidia sana akina mama, watoto na walemavu
sehemu mbalimbali, tunamuomba Baba huyu mwenye utu aje na kwetu
tunakojifungulia chini ya miembe baada ya kubebwa minzeganzega, ili
atunusuru na vifo”.alisema Selina Jovini.
Selina Jovini
ambaye Baba yake ni Mwenyekiti wa Serikali ya Kitongoji hicho kwa tiketi
Chama cha Mapinduzi (CCM) alijifungua chini ya mti huo baada ya Baba
yake Bw. Jovini Victor (54) akisaidiana na wasamari wema kumbeba kwa
umbali wa Kilomita Sita wakibakiwa na Nne ili wafike ilipo Zahanati, na
kukiri kuwa tukio hilo liliwatokea saa 10 usiku Desemba 23, 2012.
Akilikumbuka
tukio hilo Victor alisema, siku hiyo baada ya kuvuka mabonde, milima na
mito miwili mwanae alimuomba mama yake mzazi wazungumze pembeni chini ya
mti wa mwembe, ambapo alidai kwa haraka alibaini kuna jambo
limeharibika na kuwaachia nafasi, na baada ya muda mfupi alisikia sauti
ya mjukuu wa kike chini ya mwembe huo ikilia.
Victor ambaye wakati huo alikuwa anatoka kumpeleka mkewe Hosipitali
Misheni ya Bwagala kutibiwa ambayo iko kilomita zaidi ya 50 toka
Kitongoji cha Ifumbo alisema, Kero ya Barabara kwenye eneo lake bado
haijatatuliwa na wananchi wake wataendelea kupata matatizo hayo na
ikibdidi vifo, kutokana na kukosekana anayewajali ingawa eneo hilo lina
rasilimali ya madini.
Aidha Diwani
wa Viti Maalum wa Juliana Petro (CHADEMA) alisema, Kero hiyo inamkera
sana Moyoni mwake mbali ya kumnyima usingizi na hadi sasa anaumiza
kichwa chake kuona ni jinsi gani akina mama wa eneo hilo watakombolewa
na adha ya Barabara ambayo waume zao wanaendelea kung’ang’ana kuichimba
bila mafanikio, lakini alipenda serikali wilayani ikubali mawazo ya
wananchi kutaka barabara fupi badala ya ile ya mzunguko ambayo
wanaifikilia.
No comments :
Post a Comment