Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, January 10, 2013

KENYELA MGENI RASMI UBINGWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI




Kamanda wa polisi mkoa wa Kipolisi wa kinondoni Charles Kenyela anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika pambano la ngumi la kutetea ubingwa Afrika mashariki na kati kati ya bondia Mtanzania Thomas Mashali na Bernad Mackoliech wa Kenya Jumamosi katika Ukumbi wa Friends Corner Manzese.
Akizungumza na waandishi wa habari mratibu wa pambano hilo Aisha Mbegu alisema wameamua kumualika kamanda Kenyela ili kuhakikisha wanatumia nafasi hiyo kutoa Elimu ya Ulinzi shirikishi na kwa kutambua mchango wa jeshi la polisi kudumisha amani katika michezo.
“ Jeshi la polisi ni wadau wetu wakubwa katika michezo hasa ngumi na mchango wao umekuwa ukionekana kwani sasa hakuna vurugu zinazojitokeza katika mapambano yeyote ya ngumi yanayofanyika tofauti na Miaka ya Nyuma ambapo Ngumi ilikuwa Watoto hawawezi kwenda kuangalia,”alisema Aisha.
Aisha alisema katika pambano la awali ambalo lilifanyika katika Ukumbi wa Friend corner hakukuwa na vurugu na idadi ya watoto na wanawake kuangalia ngumi imekuwa ikiongezeka siku hadi siku na nhivyo kutoa hamasa kwa wazazi na watoto kupenda mchezo huo.
Mbali na Kenyela Mbunge wa Kinondoni Iddi Azan na Mbunge wa ubungo John Mnyika wamealikwa ili kushuhudia vipaji vya  vijana wa kinondoni katika Ngumi.
Bondia Mackoliech anatarajiwa kuzungumza na vyombo vya habari leo (Alhamisi) katika Uwanja wa Karume na Ijumaa wanatarajiwa kupima Uzito saa Nne asubuhi katika Ukumbi wa Friends Corner Manzese .

No comments :

Post a Comment