George Kavishe, Meneja wa Kilimanjaro Bia, wadhamini wa Kili Marathon |
KWA mara
nyingine tena kampuni ya mafuta ya GAPCO Tanzania imetambua umuhimu wa
wanariadha wenye ulemavu kwa kuwapa fursa ya kushiriki kwenye mbio za
Kilimanjaro Marathon 2013 kwa kudhamini mbio ya nusu marathon kwa ajili ya
walemavu itakayojulikana kama GAPCO GAPCO 21km Disabled Half Marathon.
Mkuu wa
Mauzo na Maskoko wa GAPCO, Ben Temu amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya
habari kuwa “Ushiriki wa wanariadha wenye ulemavu unaleta msisimko mpya kwenye
Kilimanjaro Marathon kwa mara nyingine tena. Kukimbia marathon kunaendana na
mambo ambayo GAPCO inayaamini katika shughuli zake za kila siku – mtazamo
chanya, kipaumbele katika kujiamini na azma ya kusonga mbele”.
“Ushiriki wa walemavu ni ushaidi kwamba watu
wenye ulemavu sio tu kwamba wanaweza kufanya mambo makubwa bali pia
inadhiirisha kuwa wana uwezo wa kutimiza jukumu lolote kwa ufanisi wa hali ya
juu. Kama wadhamini tunahimiza jamii nzima pamoja na makampuni mengine
yajitolee kudhamini walemavu waweze kushiriki Kilimanjaro Marathon katika siku
zijazo,” alisema.
Mbio za hizo
zitakuwa na sehemu tatu ambazo ni kiti cha magurumu (wheelchair), baiskeli ya
miguu mitatu, na walemavu wanaokimbia. Washindi watajipatia zawadi nono ambazo
jumla yake ni zaidi ya shilingi milioni 3.
GAPCO ina
nia thabiti ya kuwasaidia wanariadha walemavu ili waweze kutimiza ndoto zao na
kuthibitisha kwamba wanaweza.
Kwa mujibu
wa John Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waadaaji wa mbio hizo,
Kilimanjaro Marathon ni kati yam bio zenye mvuto zaidi duniani kutokana na kwamba
zinafanyika chini ya Mlima Kilimanjaro na ndio maana huvutia washiriki kutoka
nchi zaidi ya 40 kila mwaka. Mbio hazivutii wanariadha peke yao bali pia
watalii ambao huchangia pato la taifa”, alisema.
No comments :
Post a Comment