Marehemu Chifu Mkwawa enzi za uhai wake
|
Na Francis Godwin, Iringa
KABILA la WAHEHE
ni kama yalivyo makabila mengi ya kibantu yaliyomo nchini Tanzania,
ambao wao walikula majani, mizizi na matunda pori pamoja na vitu ambavyo
vilirithiwa vizazi na vizazi vilivyofuata na hatimaye kuwa vyakula vya
kawaida kama mizizi, miti, matunda na majani.
Mzizi wa mti wa “MTONO” huliwa
ungali bado mchanga ambao huitwa “ISONGI” unaochimbwa wakati wa masika
au mahali palipo na unyevunyevu, huliwa kama mtu alavyo muwa kwa kumenya
maganda.
Mti
wa “AMAKINGILIGITI” huzaa matunda yaliyo na sura kama “golf” matunda
haya, radha yake ni kama limao ingawa radha hiyo haijafananishwa
kisayansi, lakini hufanana na dawa za vitamini “B Complex” majani yake huliwa na mbuzi mwitu (aitwae INGULUGULU kwa lugha ya kihehe) na mbegu zake huliwa pia.
“MUTOWO”
huzaa matunda wakati wa kiangazi ambapo matunda yake huwa na nyuzi
nyuzi wakati wa kutafuna mithili ya mtu atafunaye bigijii na zikitafunwa
hutoa utomvu mzito wenye sukari nyingi, hazimezi kwa sababu zinawasha
sana kwenye koromeo na huweza kuleta kikohozi cha muda mrefu.
Aidha
mtu akila huweza kupatwa na hamu ya kiu ya kunywa maji hasa akiwa na
kazi ngumu na pia huweza kuandaliwa kwa kuchemshwa na kudumu kwa muda wa
miezi sita bila kuoza.
Matunda
“MUNYWEWA” huwa katika ganda gumu ambalo ndani yake kuna maji matamu
yanayonywewa na yanapunguza kiu yanafanana kabisa na mti wa MTANGADASI
ambao hauna maji ila una nyama nzito ambayo ni chakula kizuri cha nyani
na ngedere.
“AMAMBEDEE”
hujulikana kama tango, mmea huu hutambaa kama mmea wa maboga hupendelea
kuota zaidi kwenye mbolea ya samadi na walaji wakuu ni wenyeji wa mkoa
wa Iringa na pia huliwa na wanyamapori hada digidigi.
“MAGUHU”
mti wake ni mwepesi sana ukifananisha na MSONOBALI (CYPRESS) hustawi
sana katika mbuga za mwinuko.Wahehe huita “MUWUBAMBA” ambao hauwezi
kutumika kama kuna nishati ya kupikia kwa sababu ya wepesi wake huwaka
mfano wa karatasi, matunda yake huwa mekundu na ndani yake huwa na uji
wa rangi ya njano na ndiyo huliwa, linazo mbegu mbili zinazofanana sana
ni laini lakini haziliwi.
Upo
mti mwingine ujulikanao kama “MUFUDU” ambao huzaa matunda ya MUFUDU
ambayo huliwa baada ya kukomaa lakini yakiwa hayajakomaa yanakuwa ya
kijani huwezi kula machungu, matunda haya yana rangi nyeusi tii mithili
ya kiwi, nyama yake huwa nyeusi pia na mbegu yake hailiwi hutupwa.
Haifahamiki pia ni kwa nini Wahehe walio weusi tii hufananishwa na MUFUDU.
Inaelezwa kuwa Mtwa
GUNGIHAKA TOVELA PATELI mdogo wa Mtwa MKWAWA alikuwa mweusi tii lakini
weusi wake ulifananishwa na weusi wa NYATI wakimwita ”WUTITU WA MBOGO”
na “MUFUDU” wakimananisha ni mweusi kama NYATI na MUFUDU.
“MUSAULA”
ni mti unaofanana na miti ya MINYWEWA, MUTANGADASI, MUTUNDWA na MUGUHU
ambao huota nyanda zilizoinuka na hukomaa kiangazi tu kwa hiyo ni tunda
la msimu kati ya mwezi Mei, Juni na Julai ni chakula cha NYANI pia
huliwa na watoto wadogo zaidi.
“MUSANSAWUKI”
ni aina ya majani ambayo huota msimu wa masika tu, huzaa matunda yenye
miba mingi sana. Matunda hayo hutoa maua mengi yenye rangi nyekundu na
haya maua mekundu huwa na utomvu ambao ukifyonza ni mtamu. Utomvu huo
huitwa Wununu ambao pia huliwa na vipepeo na nyuki na watoto (binadamu).
Mizizi,
majani na matunda machache yaliyoainishwa hapo juu yalikuwa na pengine
bado yanaliwa na Wahehe kutoka siku za kale. Nia na makusudi ya kuandika
makala haya ni kukielimisha kizazi cha sasa kuwa wazazi wao walikula
vyakula hivyo vya porini ambayo vilisaidia kushinda magonjwa mbalimbali
mwilini kwa sababu vilitoa kiwango madhubuti mwilini.
No comments :
Post a Comment