Katibu mtendaji wa IPC akitoa utambulisho wa wanachama na kutoa neno la utangulizi juu ya mafunzo hayo.
MKUU wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma awataka wanahabari nchini kujikita katika uandishi wa habari za haki za binadamu na utawala bora ili
kuiwezesha jami kujua haki na wajibu wao katika maisha ya kila siku.
Mkuu
wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma alitoa rai hiyo leo katika
ukumbi wa Makitaba ya mkoa wakati akifungua mafunzo kwa
waandishi wa habari wanachama wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa
Iringa (IPC) juu ya haki za binadamu na utawala bora .
“Kupitia mafunzo haya, nendeni mkawasaidie wananchi kujua haki zao pamoja na utawala bora ili waweze kuwajibika pale
wanapotakiwa kuwajibika msiishie kuandika habari za kuwagonganisha viongozi na wananchi pekee "amesema Ishengoma.
Amessema ili jamii iweze
kujua haki zao ni lazima waandishi waelimishwe vizuri kwa kuwa wao ndio
wasambazaji wa elimu na taarifa kwa jamii.
“Wanahabari ni muhimu
sana kwa nchi yoyote ile duniani. Hii ni kwamba mwanahabari ni chombo muhimu
katika usambazaji wa elimu kwa jamii na wao ni kiungo kikubwa kati ya serikali
na jamii katika mambo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. Mwana habari ni mtu wa
kuheshimiwa kwa kuwa ni watu wakutegemewa” amesema.
Nance Ngula afisa
uchunguzi na utawala bora ambaye alikuwa mkufunzi ameseme kila mtu anahusika
katika suala zima la haki za binadamu na utawala bora kwa kuwa ndio walengwa wa
masuala hayo.
Amesema ukiukwaji wa
haki za binadamu unaweza kufanywa na mtu yeyote yule bila aidha kwa kutumia
wadhifa alio nao au kwa makusudi na kutowajibika katika nafasi.
Ngula aliwata waandishi
kuwa na utaratibu wa kuzifikia jamii na kujua changamoto wanazokabiliana nazo
na kutumia nafasi walizo nazo kwa kuwasaidia kuondokana nazo aidha kwa kutumia
elimu yao au kutafuta msaada mbadala.
Naye Shoma Philip afisa
uchunguzi mkuu wa haki za binadamu na utawala bora alisema utawala bora ni
pamoja na kuzingatia haki zote za binadamu katika ngazi zote bila kujali umri.
Amesema hata utoaji
mimba ni ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kuwa unakiuka haki ya kuishi ambayo
kila mtu anatakiwa kuipata.
“Utawala usiozingatia
haki za binadamu hauwezi kuitwa utawala bora kwani ili haki ziweze kuzingatiwa
lazima kuwepo na utawala bora” amesema.
Amesema kila wakati
migogoro mingi inasababishwa na ukosefu wa utawala ulio bora kwa kuwa haki za
binadamu zinakuwa hazithaminiwi.
Aidha amesema jamii pia
ina wajibu wa kutimiza yale ambayo yanawapasa ili kusiwe na migongano na
malalamiko kwa upande wao.
Mafunzo hayo
yaliandaliwa na kuratibiwa na idara ya haki za binadamu na utawala bora katika
serikali.
No comments :
Post a Comment