Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, January 9, 2013

KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI TIGO YAZINDUA OFA MPYA YA “TIGO TIME”



Mtaalamu wa kubuni Ofa kutoka kampuni ya simu za mkononi ya TIGO, Jacqueline Nnunduma akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.
.……………………………………………..

Tigo imetambulisha huduma mpya kwa wateja ujulikanayo kama Tigo Time, ambayo inatoa punguzo kubwa sana la gharama ya kupiga simu masaa ishirini na nne kwa wiki (24/7 ikitegemeana na muda na wakati wa siku na eneo mteja atakalokuwa.

Kusajili  huduma kwa mteja piga *149*90# au tuma neno “TIGO TIME” kwenda namba “15372” na baada ya hapo utapokea ujumbe ambao utaonyesha kwamba umefanikiwa kusajili na unaweza kuanza kutumia huduma hii na ufurahie punguzo kubwa sana la gharama. 
Baada ya kusajili, Tigo Time itakujulisha punguzo lako la gharama la kupiga simu kutokana na  muda wa siku  na eneo ulipo. Gharama ya huduma hii  ya kusajili itakuwa ni Tshs 149 kwa kiwango cha chini.

“Tigo inatambua kwamba wateja wetu wanahitaji huduma bora na kwa gharama nafuu na hii ni njia mojawapo ya kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata huduma zenye ubora wa juu na vifurushi ambavyo vitawapatia unafuu wa bei kwa muda wowote.” Alisema Bi. Jacqueline Nnunduma, Mbunifu wa ofa za Tigo. 
“Kwa punguzo hili kubwa la bei lililopita kifani, hakuna shaka kuwa Tigo Time itakuwa huduma maarufu kama ilivyokuwa huduma ya ya Kwa Sekunde tuliyoianzisha miaka kadhaa iliyopita.” Alimalizia Bi. Nnunduma. 

No comments :

Post a Comment