Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi wa klabu
ya Azam kwa timu yao kufanikiwa kutwaa Kombe la Mapinduzi mwaka huu.
Kwa
Azam kufanikiwa kutetea ubingwa huo inaonesha jinsi klabu hiyo
ilivyojipanga kabla ya kuingia katika mashindano hayo ambapo ilicheza
fainali dhidi ya Tusker FC ya Kenya.
Pia
ushindi huo utakuwa changamoto kwa timu nyingine za Tanzania Bara
zitakazopata fursa ya kushiriki michuano hiyo ya Kombe la Mapinduzi
mwakani. Michuano hiyo iko kwenye Kalenda ya Matukio ya TFF.
No comments :
Post a Comment