Jaqueline Wolpe ndio huyu
Na Mdakuzi Spesho, Dar es
Salaam
WASANII wawili maarufu hapa
nchini, Vicent Kigosi (Ray) na mwenzake Jaqueline Wolpe, siku nzima ya jana,
waliitumia katika Viwanja vya Leaders Club, huku mazungumzo yao yote yakielekea
kwa mrembwende wa zamani na mkali wa filamu Tanzania, Wema Abraham Sepetu.
Wema Sepetu akionyesha pozi lake
Hata hivyo mazungumzo hayo,
hayakuwa mabaya sana kwa wasanii hao zaidi ya kuwaza namna gani ya kulinda
majina yao yasishuke katika kipindi cha mwaka 2013 na 2014, huku mzungumzaji
mkubwa akiwa ni Ray.
Vicent Kigosi, Ray
Wakati wa mazungumzo hayo,
Wolpe alionekana kama mwenye shauku ya kutaka kufanyia kazi ushauri wa Ray,
hasa kwa kuangalia zaidi nyota ya Wema Sepetu inavyozidi kung’aa, huku kila
mmoja akitamani kumtaja au kumshika mkono.
Licha ya mazungumzo yao kuwa
siri na wakiongea kwa sauti ya chini, lakini kipaza sauti cha mdakuzi wetu
kiliwanasa na kusikia baadhi ya mambo waliyozungumza, ikiwamo ushindani wa
sanaa, hasa kwa wasichana, akiwamo Wema, Wolpe, Aunt Ezekiel na Irene Uwoya.
Kwa mwaka Wema aling’ara
sana, lakini wewe pia ulifanya kazi nzuri katika sanaa, hivyo nadhani kuna haja
ya kuongeza kasi zaidi kwa ajili ya kufika malengo,” alisema Ray, akimwambia
Wolpe aliyetega masikio yake kwa umakini.
Leaders Club hutumiwa watu
mbalimbali kujipumzisha nyakati za mchana kutokana na kuwa sehemu tulivu, jambo
linalowafanya wasanii na wengineo kukutana hapo wakibadilishana mawazo.
Makali ya Wema Sepetu
yamezidi kutishia uwepo wa wasanii wa filamu wa kike hapa nchini, kutokana na
kupendwa na watu wengi, jambo linaloongeza joto na msisimko kwa wanaofuatilia
sanaa Tanzania.
No comments :
Post a Comment