Zoezi la kuchukua na kurejesha fomu za kuwania uongozi
katika shirikisho
la soka nchini tayari limefungwa ambapo jumla wa watu 50 kati ya 52
waliochukua fomu kuomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa
huo utakaofanyika Februari 24 mwaka huu wamerejesha fomu
hizo.
Waombaji ambao hawakurejesha fomu ni Geofrey
Nyange aliyekuwa akiomba ujumbe wa Kamati ya Utendaji kuwakilisha mikoa ya
Morogoro na Pwani, na Shufaa Jumanne aliyekuwa akiomba kuwakilisha Kanda ya Dar
es Salaam.
Orodha kamili ya waombaji ambao wamerejesha fomu
ni Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi, Omari Nkwarulo na Richard Rukambura (Rais).
Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia (Makamu wa
Rais).
Kwa upande wa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni
Abdallah Musa, Salum Chama na Kaliro Samson (Kagera na Geita), Jumbe Magati,
Mugisha Galibona, Richard Rukambura, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus
Lufano (Mara na Mwanza).
Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na
Simiyu), Charles Mugondo, Elly Mbise na Omari Walii (Arusha na Manyara), Ahmed
Mgoyi na Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Blassy Kiondo,
Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama na
Stanley Lugenge (Njombe na Ruvuma).
Athuman Kambi, Francis Ndulane na Zafarani
Damoder (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida),
Farid Nahdi, Hassan Othman Hassanoo, Riziki Majala na Twahili Njoki (Morogoro na
Pwani), David Lugenge, Elias Mwanjala, Eliud Mvella na John Kiteve (Iringa na
Mbeya), Davis Mosha, Khalid Mohamed na Kusiaga Kiata (Kilimanjaro na Tanga) na
Alex Kamuzelya, Juma Pinto, Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir na Shaffih Dauda
(Dar es Salaam).
6 WAOMBA
UONGOZI BODI YA LIGI KUU, WOTE WAREJESHA
FOMU
Waombaji
wote sita wa uongozi katika Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) ambayo uchaguzi wake
utafanyika Februari 22 mwaka huu wamerejesha
fomu.
Kwa
upande wa Mwenyekiti waombaji ni Hamad Yahya wa Kagera Sugar na Yusuph Manji wa
Yanga wakati Makamu Mwenyekiti aliyeomba ni Said Mohamed wa
Azam.
Nafasi
mbili za ujumbe wa Bodi ya Ligi Kuu kwa klabu za Daraja la Kwanza zimeombwa na
watu watatu. Waombaji hao ni Christopher Peter Lunkonde wa Moro United, Kazimoto
Miraji Muzo wa Pamba ya Mwanza na Omari Khatibu
Mwindadi.
Kamati ya
Uchaguzi ya TFF itaanza kukutana kesho kwa ajili ya kupitia fomu zote
zilizowasilishwa na waombaji kwa ajili ya uchaguzi wa TFF na ule wa Bodi ya Ligi
Kuu.
No comments :
Post a Comment