DAR ES SALAAM, Tanzania
Mbio za Kilimanjaro Marathon mwaka huu zinatajiwa kuwa na washiriki wa kigeni wapatao 600 kutoka nchi zaidi ya 40.
John Addison,
Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo alisema katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari jana kuwa mbio hizo zinaendelea
kuwavutia washiriki wengi wa kimataifa kutokana na jitihada za pamoja
zinazofanywa na waandaaji pamoja na bia ya Kilimanjaro Premium Lager
katika kutangaza tukio hili. Hii ndi sababu iliyochangia ukuaji wa mbio
hizi pamoja na ushiriki kuongezeka kila mwaka.
Addison
alisema washiriki wengi zaidi watatoka Marekani ikifuatiwa na Uingereza.
Nchi nyingine zinazotarajiwa kushiriki ni pamoja na Canada, Japan,
Uganda, Zimbabwe na Kenya. Nyingine ni pamoja na Sweden, Australia,
Hungary, Germany, Zambia, Morocco, Swaziland, Nigeria na Malawi.
Zikiwa
zimepangwa kufanyika Moshi tarehe 3 Machi 2013, mbio za Kilimanjaro
Marathon zitakuwa zimegawanyika katika sehemu nne ambazo ni 42km
Kilimanjaro Premium Lager Marathon, 21km Half Marathon, GAPCO Disabled
Half Marathon na Vodacom 5km Fun Run.
Mbio hizo pia
zinatarajiwa kuchangamshwa na ushiriki wa timu za makampuni ambapo
wafanyakazi wa makampuni wadhamini watashindana katika mbio ya nusu
marathon kupitia shindano litakalojulikana kama“Half Marathon Corporate
Challenge”.
Makampuni
ambayo yameishathibitisha kushiriki shindano hilo ni pamoja na TPC Sugar
ambao ndio mabingwa watetezi wa shindano hilo wakifuatiwa na CFAO
Motors, TanzaniteOne na Tanga Cement.
Addison
alisema kuwa mbio za Kilimanjaro Marathon zinaingia katika mwaka wa 11
tangu kuanzishwa zikiwa zimesajiriwa rasmi na shikisho la riadha la
kimataifa na kuongeza kuwa kutakuwepo na vituo vya maji pamoja na
viburudisho katika njia ya mashindano hayo.
“Mbio hii
inafanyika chini ya Mlima Kilimanjaro ambapo kila mtu anaweza kukimbia
kwa raka kwani urefu wake kutoka usawa wa bahari ni wastani wa mita 830
mpaka 1150 katika barabara nzuri yenye lami. Inatarajiwa kuwa
shamrashamra maana wananchi wengi watajitokeza pembezoni mwa barabara
kuwashangilia na kuwapa moyo wakimbiaji, na wakimbiaji wa kujifurahisha
wanaweza hata kusimama kupata kiburudisho njiani”, Addison aliitimisha.
Mbio hizo
zinadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager (wadhamini wakuu), Vodacom
Tanzania (5km Fun Run), GAPCO (Disabled Half Marathon), Tanga Cement,
CFAO Motors, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne, New
Arusha Hotel na Kilimanjaro Water.
No comments :
Post a Comment