Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko
ya Katiba Jaji Jospeh Warioba (kulia) akiongea na Mawaziri leo katika
ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam katika mkutano
uliolenga kupata maoni ya Mawaziri kuhusu Katiba Mpya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na
Uvuvi Dkt. Charles Nyamrunda akiongea katika mkutano kati ya Tume ya
Mabadiliko ya Katiba na Makatibu Wakuu uliolenga kupata maoni yao kuhusu
Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini
Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Makatibu Wakuu wa Wizara
mbalimbali wakifuatilia mkutano kati yao na Tume ya Mabadiliko ya
Katiba uliolenga kupata maoni ya Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu
Wakuu kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa
Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni
Sefue akiongea katika mkutano kati ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na
Makatibu Wakuu uliolenga kupata maoni yaokuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo
ulifanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.
Mawaziri Steven Wassira, Kapteni
(Mstaafu) George Mkuchika na Prof. Sospeter Muhongo wakifuatilia mkutano
kati yao na Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliolenga kupata maoni ya
Mawaziri kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa
ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Angellah Kairuki akiongea katika mkutano kati ya Mawaziri, Manaibu
Mawaziri na Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliolenga kupata maoni ya
Mawaziri kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa
ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali
(Mstaafu) Joseph Simbakalia akiongea katika mkutano uliofanyika katika
ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo kati ya Tume ya Mabadiliko ya
Katiba na Wawakilishi wa Wakuu wa Mikoa uliolenga kupata maoni yao
kuhusu Katiba Mpya. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw.
Abass Kandoro, Dkt. Rehema Nchimbi (Dodoma) na Bi. Chiku Galawa (Tanga).
Wawakilishi wa Wakuu wa Mikoa
nchini wakipata maelezo kuhusu mfumo wa uhifadhi wa maoni ya wananchi
kuhusu Katiba Mpya yanayowasilshwa katika Tume kwa maandishi kutoka kwa
Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume Bi. Flora Mkonya leo (Jumanne, Jan 15,
2013) katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia Kanali
(Mstaafu) Joseph Simbakalia(Mtwara), Bw. Abass Kandoro (Mbeya), Bi.
Chiku Galawa (Tanga).na Dkt. Rehema Nchimbi (Dodoma).Wakuu hao wa mikoa
pia waliwaslisha maoni ya Wakuu wa Mikoa kuhusu Katiba Mpya.
Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba Bi. Al-Shymaa Kway-Geer, Bw. Humphrey Polepole na Bi. Riziki
Mngwali wakifuatilia mkutano kati ya Tume na Mawaziri uliolenga kupata
maoni ya Mawaziri kuhusu Katiba Mpya. Mkutano huo ulifanyika katika
ukumbi wa ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam leo.
No comments :
Post a Comment