Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, January 30, 2013

"SIKUENDA UINGEREZA KUUZA SURA.." IRENE WOYA






MSANII mahiri wa filamu Irene Uwoya, ameamua kuweka wazi kuwa safari yake aliyowahi kuifanya ya nchini Uingereza mwaka jana kwa ajili ya mazungumzo ya kufanya filamu ya kimataifa bado hayajazaa na matunda na hadi sasa wapo kwenye mazungumzo.

Kauli ya msanii huyo ilimfanya mwandishi wetu amdadisi zaidi, ambapo alisema kuwa kwa sasa kitu wanachokizungumzia ni namna watakavyoandika story ingawa hakutaka kuweka wazi ni story ya namna gani.

Hata hivyo alisema kuwa bado hawajafikia mazungumzo ya kulipwa kiasi gani na lini watafanya lakini anaamini kila kitu kitakuwa safi kwani watu hao wameonesha nia ya kufanya nae kazi.

Pamoja na hayo alishindwa kuwaweka wazi watu hao hata kwa kuwataja majina, kwa madai kuwa kwa sasa siyo wakati wake kwani muda ukifika mashabiki wake watajua anaenda kufanya kazi na kampuni gani.

“Bado tunaendelea na mazungumzo.Sikuenda huko kuuza sura .Najua watu wanasubiri kuona ukweli juu ya maneno yangu haya lakini nachotaka kusema ni kwamba ni kweli nilienda kwa ajili ya mazungumzo ila bado mambo hayajakaa sawa,” alisema Uwoya

No comments :

Post a Comment