Tingatinga likivunja sehemu ya nyuma ya nyumba hiyo. |
Kazi ya kubomoa jengo hilo ikiendelea chini ya usimamizi wa Kampuni ya Udalali ya Rhino Auctionmart. |
Kutokana na kuta za nyumba hiyo kuwa ngumu kazi ya ubomoaji ililazimika kuanzia madirishani ili kurahisisha ubomoaji. |
Nyumba hiyo ikiondolewa milango mapema kabla haijaanza kuvunjwa. |
ALIYEKUWA Rubani wa ndege ya Rais kwa awamu zote nchini Kapteni Felix Kileo,
leo ameondolewa kwa nguvu ndani ya nyumbayake na kubomolewa na Kampuni ya
Udalali ya Rhino Auctionmart, huku kukiwa na madai ya kuwepo kesi mahakamani
inayoendelea.
Kwamujibu wa wabomoaji hao wanadai
kuwa wamepata idhini ya kubomoa nyumba hiyo kutoka kwa Taasisi ya Benki ya
Wakulima (TIB) ambayo inakusudia kujenga Ghorofa kwenye eneo la nyumba hiyo
lililopo mtaa wa Ohayyo kitalu namba 15.
Ndugu wakaribu wa Kapteni huyo ambae
mwenyewe hakuwepo kwa muda huo eneo la tukio wamelalamikia kitendo anachofanyiwa
nduguyao hasa ukizingatia ni mtumishi wa siku nyingi wa
serikali.
“Huyu mimi ni nduguyangu amekuwa
mtumishi wa serikali za awamu zote amestaafu mwaka jana kama rubani wa ndege ya
Rais lakini anachofanyiwa ni udhalilishaji, na vitendo hivi si vya kistaraabu
hata kidogo ni ufisadi tu huu, pesa zitatoa roho ya mtu hi!” alisikika mmoja wa
kaka wa Kapteni huyo.
Kwamujibu wa ndugu hao kesi ya msingi
iko mahakamani na keshokutwa inasikilizwa lakini wameshangazwa kitendo cha
kuwavamia bila hata barua ya mahakama na kuvunja nyumba hiyo.
Taarifa ilizozipata blog hii kutoka
eneo la tukio nikwamba mtumishi huyo wa Serikali alitakiwa kuhama kwenye nyumba
hiyo ili kupisha ujenzi wa jingo la Benki hiyo nayeye kupewa nyumba nyingine
yakuishi lakini alikataa na upande wa Serikali kufungua
kesi.
Baada ya kufunguliwa kesi upande wa
serikali ulishinda lakini Kapteni huyo kupitia mawakiliwake walikata rufaa
iliyosabisha zoezila kuendeleza kiwanja hicho
kusimama.Chanzo : NdgShilatu Blog.
No comments :
Post a Comment