ZittoKabwe
“
Dar inachangia asilimia 80 ya mapato.
Kitovu cha Uchumi. Darinachangia 90% ya ufisadi.
Uti wa mgongo wa ufisadi nchini”
Malumbano kati ya wananchi wa Mtwara na
Serikali kuhusu matumizi boraya utajiri wa nchi yameendelea kwa takribani wiki
moja sasa.Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Waziri wa Nishati na Madinikuwaita
Watanzania wa Mtwara Wahaini, wapuuzi na watu hatari, Rais waJamhuri ya
Muungano wa Tanzania naye aliingia kwenye mjadala huo kwakuonya watu
wanaowaunga mkono watu wa Mtwara na kuwaita watuwanaotafuta umaarufu wa kisiasa
na wanaotaka kugawa nchi.Siku moja baada ya hotuba ya Rais, Waziri wa Nishati
na Madini alifanyamkutano na waandishi wa habari kueleza suala lile lile ambalo
bosi wakealilielezea usiku wa kuamkia mwaka mpya 2013. Hii ni dalili ya
Serikalikuweweseka.Katika kauli ya Serikali, ambayo haikuwa na jipya zaidi ya
wimbo ule ule wa
‘kugawa nchi’ ‘umaarufu wa kisiasa’ nk,
Serikali ilitaka kuonyesha ummakuwa watu wa
Mtwara hawana shukurani.Kwamba miaka yote toka Uhuru watu wa Mtwara wamekuwa
wakilishwana Pamba, Kahawa, Chai, Tumbaku, Sukari, Kidatu nk. Kwamba watu
waMtwara na Lindi hawakuchangia hata kidogo kwenye hazina ya Taifa. Hivyowao
kupigia kelele gesi yao ni uchoyo na roho mbaya na kukosa shukurani.
Kauli ya Serikali ni kauli ya chombo
kinachoendelea kukosa ‘legitimacy’ ya
kuongoza taifa. Ni kauli ya kukata tamaa.
Ni kauli hatari sana dhidi yaWatanzania waliojitolea damu kulinda uhuru wa nchi
yetu.Moja, Serikali katika kauli yake haitaji kabisa kwamba toka Uhuru watu
waMtwara na Lindi wamekuwa wachangiaji wakubwa sana katika uchumi waTaifa
kupitia zao la Korosho.Takwimu za Uzalishaji wa Korosho zinaonyesha kwamba
kuanzia mwaka1965 mpaka 2011 Korosho imeliingizia Taifa fedha kigeni jumla ya
dola zaKimarekani 4.58 bilioni ( Cashewnuts Sub-sector study 2003, Hali
yaUchumi 2012, Cashewnuts Tanzania Report 2010).Katika Mwaka wa Uchumi
unaoishia Novemba 2012, Korosho imeliingiziaTaifa jumla ya dola za Kimarekani
151 milioni. Katika mwaka 2011 zao hilililiingiza dola 130 milioni wakati Pamba
iliingiza dola 53 milioni tu.Licha ya Zao la Korosho kuingiza fedha hizi za
kigeni (sawa ni shilingitrilioni 7.2) kwa nchi mikoa ya Lindi na Mtwara ipo
miaka 50 nyumakimaendeleo kulinganisha na mikoa mingine ya Tanzania.Serikali
inataka kufuta historia ya mchango wa zao la Korosho kwenyeuchumi wa nchi yetu
kwa sababu ya uroho wa gesi asilia. Kwa nini kaulirasmi ya Serikali haijataja
Korosho kabisa?Kauli hii ilipitishwa na ngazi zote za Serikali? Mawaziri wa
Serikaliwanaotoka mikoa ya Lindi na Mtwara walikubali kauli kama hii itoke
dhidiya wananchi wao wanaoteseka na zao la Korosho miaka nenda miaka rudi?Pili,
Serikali imesahau kabisa mchango wa watu wa Lindi na Mtwara katikaulinzi wa
Taifa letu. Moja ya sababu ya mikoa ya Lindi na Mtwara kuwanyuma kimaendeleo ni
juhudi za ukombozi wa kusini mwa Afrika.Kambi ya wapigania uhuru wa Msumbiji
ilikuwa Nachingwea. Kambi yaFrelimo iliwekwa kwenye Shamba la Mkonge kilometa
17 tu kutoka mjiniNachingwea ambapo ilikuwa makao makuu ya ukombozi wa
Msumbiji. RaisSamora Machel, Rais Joaqim Chissano na Rais Guebuza
waliendeshamapambano kutoka kusini mwa Tanzania.Makaburu wa Afrika Kusini na
Wareno walikuwa wanashambulia nchi yetu
na mikoa hii miwili ya Lindi na Mtwara
ikawa ‘buffer zone’. Wakati Dar es
Salaam inaendelea kwa kila aina ya
maendeleo, mikoa ya Lindi na Mtwarailikuwa inalinda ili wanaoishi Dar es Salaam
na mikoa mingine waishi waamani na starehe. Serikali inapimaje mchango huu wa
mikoa hii?
Tunaipima kwa fedha? Uroho wa gesi asilia
kuzalisha umeme wakufurahisha walalaheri asilimia 14 nchini ndio inaifanya
Serikali kusahau
kabisa ‘sacrifice’ ya watu wa Mt
wara katika kulinda uhuru wa Taifa
letu?Tatu, Serikali inasema lazima bomba lije Dar es Salaam kwa sababu Darndio
inazalisha asilimia 80 ya Mapato ya Serikali. Kwanza huu ni uwongo.Ni aibu
Serikali kujitetea kwa uwongo. Dar es Salaam ni kituo tu chakukusanyia mapato
ya Serikali. Uzalishaji mkubwa wa nchi yetu wenyekuzalisha kodi unafanyika nje
ya Dar es Salaam.Walipa kodi wakubwa wengi Ofisi zao Kuu zipo Dar es Salaam
lakiniuzalishaji wao unafanyika nje ya Dar es Salaam. Serikali itoe orodha
yawalipa kodi wakubwa 100 tuone uzalishaji halisi wa mapato hayounafanyika
wapi.
Hata hivyo inawezekana kuwa ikawa kweli Dar
es Salaaminakusanya asilimia 80 ya mapato ya nchi.Basi na tuseme Dar es Salaam
inachangia asilimia 90 ya ufisadiwote nchini. Kashfa zote kubwa za Ufisadi
zinafanyika Dar esSalaam na fedha nyingi za ufisadi zinatumika Dar es Salaam.
Mwisho, maandamano ya watu wa Mtwara ni
kielelezo tosha kwamba watuwa mikoa ya Lindi na Mtwara wamechoshwa na
longolongo za Serikali.Wananchi wa Mtwara na Lindi wanataka Uwajibikaji wa
Serikali kuhusuutajiri wa nchi. Mtanzania yeyote mwenye tahadhari ya nchi yetu
kutokuwana laana ya rasilimali ataungana mkono na watu wa Lindi na Mtwara
kudaimaendeleo.Nilitoa mfano wa Mgodi wa Golden Pride ambao umemaliza dhahabu
yotetani 76 katika eneo la Lusu wilayani Nzega.
Kampuni ya Resolute ya Australia iliwekeza
dola 370 milionikuanzia mwaka 1998 (mkataba wao ulisainiwa 25th June
1997).Katika kipindi cha uhai wa mgodi, miaka 14, Kampuni hii imeuzadhahabu ya
thamani ya dola za kimarekani 3.3 bilioni.Kabla Serikali haijawaita watu Mtwara
wahaini, wapuuzi na watuhatari, iwaambie watu Watanzania kodi kiasi gani
imekusanywakutoka mgodi huu katika kipindi cha miaka 14.Mpaka mwaka 2008, kwa
mujibu wa Taarifa ya Kamati ya Bomani,kampuni hii ilikuwa imelipa mrahaba wa
dola 11 milioni na kodi
|
No comments :
Post a Comment