Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa BMT Henry Lyhaya amewataka viongozi na wagombea Uongozi wa Shirikisho wasiharishe tena tarehe Mpya ya uchaguzi walioipanga.
Akiongea na kipindi cha Michezo na Burudani Katibu Lyhaya amesema hii ni mara ya tatu kuharishwa kwa uchaguzi kutokana na sababu mbalimbali.
Amefahamisha kwamba sababu nyingine ni za msingi lakini si busara kuendelea kuvunja ni bora wafanye jitihada za makusudi ili wamalizane na suala la uchaguzi huo.
Hapo awali uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Oktoba 16 baadaye Oktoba 23, Oktoba 30 na sasa wamepanga Novemba 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kuchelewa kwao kufanya uchaguzi kunanyima fursa ya kufanyika uchaguzi katika mikoa ambayo hadi hii leo bado hawajafanya.
Vyama ambavyo vimeshafanya uchaguzi ni Ruvuma, Tanga, Mara, Arusha huku Chama cha Mchezo huo Mkoa wa Dar es Salaam wao wamepanga kufanya uchaguzi wa kubadirisha Uongozi Decemba mwaka huu
MAKALLA,LAIZER WAZINADI FURSA ZA UTALII NA UWEKEZAJI NGORONGORO
-
Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Huduma za Shirika Ngorongoro Bw. Aidan Makalla
(kulia) akiwa ameambatana na Abdiel Laizer Afisa Utalii Mkuu Msaidizi
amekutan...
3 hours ago
No comments :
Post a Comment