Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, November 10, 2009

MKWASA AKABIDHIWA MIKOBA AFRICAN LYON

Baada ya Timu ya soka ya Afrikan Lyon inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara Jahazi lake kuelekea kuzama ikiwa ni ya pili toka mkiani ikiwa na pointi zake Saba, Uongozi wa klabu hiyo imemsainisha mkataba Kocha mkuu wa timu ya taifa ya wanawake Charles Bonifasi Mkwassa ili kuinusuru timu hiyo ili isishuke daraja.
Akizungumza na kipindi cha michezo na burudani Msemaji wa Afrikan Lyon Hassan Mvula amesema wanaufahamu uwezo wa Mkwassa na ndiye atakayeliokoa jahazi hilo lisizame.
Mvulla amesema wanaamini uzoefu wa ligi ya soka Tanzania aliyonao Mkwassa pamoja na uzoefu wake katika timu ya taifa ya wanawake utaisaidia klabu hiyo kuhakikisha wanabaki ligi kuu.
Naye Kocha Boniface Mkwassa amesema atafanya jitihada za maksudi ili kuhakikisha mzunguko wa ligi kuu unamalizika na timu ya Afrikan Lyon inabaki katika nafasi yake.
Amekiri anajukumu la kuifundisha timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania ambayo inajiandaa na michuano ya nchi za Magharibi mwa Afrika, lakini endapo atapatikana mtu mwingine wa kuifundisha timu ya taifa ya wanawake yuko tayari kuachia ngazi.
Amesema licha ya mapenzi yake katika kufundisha soka la wanaume, lakini michezo hivi sasa ni ajira hivyo swala la maslahi ni muhimu kwa mwanamichezo yeyote, hivyo naye amekwenda African Lyon kufuata donge nono la fedha.

No comments :

Post a Comment