Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, November 6, 2009

GURUMO NI MWANACHAMA WA SIMBA - AKABIDHI ZAWADI BAADA YA KUICHAPA YANGA

Mwanachama wa Klabu ya simba,Muhidini Gurumo (kushoto) akimkabidhi baadhi ya CD ,Kocha wa timu ya Simba, Patric Phiri, baada ya kukunwa na ushindi wa timu hiyo dhidi ya watani wao wa jadi Yanga, CD hizo ni albam tano tofauti tofauti za bend ya Msondo music pamoja na matunda mbalimbali vyenye thamani ya shilingi laki moja alivikabidhi Dar es salaam, anae shughudia katikati ni kocha msaidizi wa timu hiyo, Amri Saidi.(Picha na Rajabu Mhamila)Hapa Kamanda Gurumo anabadilishana mawazo na kocha Phiri, kama anamwambia vile "waambie wachezaji wako washambulije kama msondo wanavyoshambulia jukwaa"Kocha msaidizi wa Klabu ya Simba Amri Saidi (kulia) na dereva wa gari ya Msondo Muddy wakibeba matunda aliyoyaleta Gurumo ikiwa ni sehemu ya zawadi kwa klabu hiyo.
Simba hadi sasa inaongoza msimamo wa kundi ikiwa imejikusanyia jumla ya pointi 30 katika michezo kumi iliyocheza, ikiwa na rekodi ya kutopoteza mchezo hata mmoja katika ligi kuu Tanzania bara msimu huu.
Wakati huo huo BENDI ya muziki wa dansi ya Msondo Ngoma (Msondo(Music Band) inatarajia kufanya shoo kubwa ya kuitambulisha albamu yao mpya itakayotambulika kwa jina la 'huna Shukrani' tarehe 27 mwezi huu kabla ya uzinduzi wake utakaofanyika mapema mwaka huu.
Utambulisho wa albamu hiyo utakwenda sambamba na utambulisho wa wanamziki wapya wa bendi hiyo walioingia hivi karibuni Edo Sanga na Rashidi Mwizingwe.
Akizungumza Dar es Salaam,Meneja wa bendi hiyo Said kiberiti alisema oneshoo hilo litakuwa maalumu kwa ajiri ya kuwaweka sasa wapenzi wa bendi hiyo ili waweze kuipokea albamu hiyo mpya yenye nyimbo saba.
Alisema kutokana na kuwa kimya kwa mda mrefu mashabiki wao watakuwa wamekata tamaa kwa hiyo wameadaliwa shoo hiyo ili waweze kuburudika nao kabla ya uzinduzi wake.
''Tumeadaa onyesho maalumu litakalofanyika hapa Dar es Salaam katika ukumbi utakaotajwa baadaye ili mashabiki wetu waamke wasifikiri kama tumewaacha na pia siku hiyo tutawatambulisha tena wasanii wetu ambao tumewapokea mwaka huu,'' alisema Kiberiti.
Alizitaja nyimbo zitakazokuwa katika albamu yao ni Huna shukrani ulioimbwa na (Saidi mabela),cheo ni Dhamana(Edo sanga),Kiapo(hussein Jumbe),Mama kosi(Joseph Mahina)Haki yangu iko wapi(Huruka Huvuruge),Kimya kingi(Dj Papa) pamoja na Albino ulioimbwa na wanamziki wote wa bendi hiyo.
Kiberiti alisema pia kutakuwa na kikundi kingine kitakachosindikiza onesho hilo ambacho kinaandaliwa na kitatangazwa kwa wapenzi kabla ya oneshoo kufanyika.
Mbali na maandalizi ya albamu yao hiyo Kiberiti alifafanua kuwa bendi hiyo imeanza maandalizi ya utunzi wa nyimbo mpya ambazo zitakuwa maalumu kwa ajili ya mwaka ujao wakiwa na lengo la kuendeleza burudani kwa mashabiki wao.

No comments :

Post a Comment