Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, November 18, 2009

KOMBE LA DUNIA TANZANIA

Meneja Masoko wa CocaCola, Rita Tsehai akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu ratiba na utaratibu utakaotumika wakati wa ujio wa Kombe la Dunia linalowasili leo Jijini.Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Fredrick Mwakalebela.
WAZIRI wa Habari Utamaduni na Michezo George Mkuchika anatarajiwa kuiwakilisha Serikali wakati kombe halisi la Dunia litakapowasili leo kwenye uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa katika ziara ya kuzitembelea kila nchi ya Bara la Afrika chini ya udhamini wa kampuni ya CocaCola.Kombe hilo ambalo ni alama kuu ya michezo nikielelezo cha ubora wa soka dunia ni linatarajiwa kutua nchini kuanzia majira ya saa 10 jioni na kualakiwa na na viongozi mablimbali wa SErikali na Shirikisho la soka nchini pamoja na mashabiki wa mchezo wa soka.
Akizungumza Dar es Salaam jana Meneja Masoko wa kamuni ya Coca Cola Tanzania Rita Tseai alisema kampuni hiyo imejiandaa kuchangamsha mapokezi hayo ambayo yatapambwa na burudani mbalimbali kwa ajili ya kuongeza hamasa kwa wapenzi wa mchezo wa soka.
"Kutokana na hamasa inayotaokna na kombe hili ambayo ni nembio kuu ya soka Dunia, Coca Cola inafanya kazi kwa karibu na maafisa wa uwsanja wa ndegewa Mwalimu Nyerere na wahusika wengine kuhakikisha uwsalama unakuwepo na kuifanikisha ziara hii kwa ujumla", alisema.
Alisema likiwa nchini maelfu ya mashabiki wanatarajia kujitokeza kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na viwanja vya Forodhani, Zanzibar kuliona kombe hilo na kupiga nalo picha ambapo pia aliongeza kuwa watapata nafasi ya sinema maalumu ambayo itakuwa ikionyesha matukio kadhaa muhimu ya kukumbukwa ya kombe la Dunia la FIFA na burudani nyingine nyingi.
"Baada ya kuwasili kombe hilo siku ya itakayofuata (ijumaa) litakuwa hapa uwanja wa Taifa kwa ajili ya mashabiki wa soka kuja kuliona na kupiga nalo picha ambapo kwa upande wa uwanjani mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali", alisema
Alisema sehemu ya kwanza ya ziara ya kombe hilo itafika kilele Desemba 3 mwaka huu huko Cape Town , Afrika Kusini ambapo ratiba ya mwisho ya fainali za kombe la Dunia za mwaka 2010 itapangwa kwa tena kwa mara ya pili mwezi januari kwa ajili ya katika nchi kadhaa duniani ambapo itafikia kilele chake mwezi Aprili mwakani.
Alisema ya kombe hilo kwa mwaka huu ni ndefu zaidi duniani ambapo FIFA ikishirikian na kampuni ya Coca Cola italitembeza kombe hilo halisi katika mataifa 86 ziara ambayo itachukua siku 225.

No comments :

Post a Comment