Akizungumza na Waandishi wa Habari katika ofisi ya TFF Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho hilo Sunday Kayuni ametanabaisha kuwa walipata barua kutoka Chama cha soka cha Zanzibar ZFA kwa Timu zao kushindwa kushirikishwa katika michuano hii hivyo TFF imekiri kuteleza na kuamua kuwapa nafasi hiyo Timu ya Mafunzo.
Kayuni ameongeza kuwa tayari Timu mbili toka Kenya zitakazoshiriki michuano hiyo ambazo ni Sofapaka ambao tayari wamekwishatangaza ubingwa wa ligi kuu nchini Kenya na Tusker na kufikisha jumla ya Timu sita zitakazoshiriki kwenye Mashindano hayo.
Lakini wakati TFF ikiiteu timu ya Mafunzo kushiriki michuano ya kombe la Tasker, Mwenyekiti wa Timu ya JKT Ruvu Meja Charles Mbuge amesikitishwa na Uamuzi huo na kusema kuwa TFF wanapepesuka katika kufikia maamuzi yao.
Wakati huo huo Shirikisho la soka la Tanzania TFF linaendendelea kuwakumbusha Vilabu vyote hapa Nchini kutumia kipindi cha usajili ipasavyo badala ya kuchelewa na kuleta matatizo hapo baadae.
Sunday Kayuni Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF ameyasema hayo kwenye Ofisi za Shirikisho hilo kuwa kila mara wanapokea simu kutoka sehemu mbali mbali wakiulizia juu ya Usajili utaanza lini na kumalizia lini.
No comments :
Post a Comment