Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, November 10, 2009

ZANTEL WAZINDUA HUDUMA MPYA

Mkuu wa Mauzo wa Kampuni ya Zantel Bw. John Mbaga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam, kuusu huduma mpya ya viwango vya sh. 1 na SMS za bule zilizozinduliwa, kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Bihashara wa Kampuni hiyo Bw. Fintan Lawler.(Picha na Rajabu Mhamila)

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zanziba Telecom Ltd (Zantel) imezindua huduma mpya ijulikanavyo kama Tsh 1 + Sms za bure inayowapa wateja wa mtandao huo malipo kabla ya wanaotumia viwango hivyo kwa sekunde.
Akizindua huduma hiyo Dar es Salaam kwa waandishi wa habari,Mkuu wa Mauzo Bw.John Mbaga amesema kuwa Zantel imeamua kuzindua huduma hiyo kwa wateja wake ili kutimiza ahadi zake walizoahidi awali na kuwapa fursa za kuendelea kutimia mtandao huo.
Bw.Mbaga amesema kuwa mpango huo utaendelea kuwawezesha wateja wake kuongea zaidi na kujipatia Sms za bure zitakazowawezesha kuwasiliana na ndugu,jamaa na marafiki kwa muda wa mchana na usiku."Wateja wetu watafaidika na sms za bure zaidi kwa kila siku kwenda mtandao wa Zantel au mitandao mingine na azma yetu ni kuweka watu karibu,pia tunawakaribisha wateja wapya kujiunga katika huduma hiyo,"amesema.
Amesema kuwa kampuni ya Zantel imejitolea kuhakikisha inaendelea kutoa huduma bora kwa watanzania kwa bei nafuu na inaamini kuwa mtandao huo ndio wa kwanza na wa kipekee Tanzania kutoa sms za bure.

No comments :

Post a Comment