Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, November 13, 2009

SIJASHINDWA NIMETOLEWA - ELIZABETH

Aliyekuwa mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Big Brother, Elizabeth Gupta,(kushoto)akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam kuusu mashindano hayo kulia ni Meneja mwendeshaji, Ronald Shelukindo.(Picha na Rajabu Mhamila)

MWAKILISHI wa Tanzania katika mashindano ya Big Brother, Elizabeth Gupta, amesema kuwa kila kitu mtu akitaka kufanya kwa ajili ya mafanikio, anaweza kutimiza malengo yake.
Akizungumza Dar es Salaam, Elizabeth alisema kuwa licha ya kutoka katika jumba hilo nchini Afrika Kusini, bado ataonekana kuwa mmoja wa wanawake waliofanya vizuri katika mashindano hayo lakini bahati haikuwa yake.
Alisema kuwa ametoka katika jumba hilo ikiwa ni siku 63 tangu aingie, lakini amejitahidi kadri ya uwezo wake na anatarajia kufanya vizuri zaidi katika miaka ijayo.Elizabeth alisema kuwa imekuwa ni vigumu sana kwa yeye kuibuka na ushindi kutokana na mwaka huu sheria mbalimbali zimebadilika ikiwa ni pamoja na nchi nyingine kuwakilishwa na zaidi ya watu wawili.
"Nafurahi sana kurudi nyumbani salama, nimeweza kufanya vizuri kadri ya uwezo wangu hivyo natarajia kufanya vizuri zaidi katika miaka ya karibuni, hata kama sijabahatika kuwa mshindi wa kwanza katika jumba la Big Brother, bado mie najiona mshindi" alisema Elizabeth.
Alisema kuwa anatarajia kutafuta chuo kwa ajili ya kujiendeleza katika sanaa na hivyo anaahidi kufanya mabadiliko makubwa katika medani hiyo.
Elizabeth aliwasili nchini jana usiku akitokea Afrika Kusini baada ya kutolewa katika jumba la Big Brother.

No comments :

Post a Comment