Katibu mkuu wa Chama cha Makocha hapa nchini TAFCA Egini Mwasamaki ameomba watanzania wakae kimya na waache kumuingilia kocha mkuu Mbrazil Maxio Maximo ili afanye kazi yake vizuri.
Akizungumza na kipindi cha michezo cha Radio Times FM Mwasamaki amesema Maximo yeye ni kocha ambaye anaifahamu vyema kazi yake na mchezo iliyochezwa Misri na Yemeni ni majaribio na si ushindani hivyo si lazima timu ifunge.
Aidha ameongeza kwamba kitendo cha kumkosoa na kumzomea hakijengi ila anapofanya vizuri pia asifiwe na ushauri si lazima haupokee na kuufanyia kazi bali silaha ya kufundiosha anayo mwenyewe.
MAKALLA,LAIZER WAZINADI FURSA ZA UTALII NA UWEKEZAJI NGORONGORO
-
Naibu Kamishna wa Uhifadhi, Huduma za Shirika Ngorongoro Bw. Aidan Makalla
(kulia) akiwa ameambatana na Abdiel Laizer Afisa Utalii Mkuu Msaidizi
amekutan...
3 hours ago
No comments :
Post a Comment