
Fredrick Mwakalebela ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka Nchini TFF ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika ofisi za Shirikisho kuwa vigezo vilivyotumika kuteua vilabu hivyo ni kutokana na msimamo wa Ligi kuu unavyoendelea kwa sasa kwa Timu hizo kushika nafasi za juu.
Klabu zilizochaguliwa kushiriki michuano hiyo ni Simba, Yanga, Azam FC na Mtibwa Suger.
Klabu hizo za Ligi kuu Tanzania Bara zimetakiwa kujiandaa mapema kabla ya kuanza kwa Mashindano ya Tusker Challenge Cup litakapoanza kurindimba hapo Decemba 14 hadi 27 jijini Dar es Salaam mwaka huu.
Wakati huohuo Afisa Masoko wa Tusker ambao ni wadhamini wakuu mashindano hayo Gasto Lyaruu amekabidhi hundi ya kiasi cha shilingi milioni thelathini kwa Shirikisho hilo na kusema wametoa fedha hizo kwaajili ya kuanza kufanya maandalizi mapema ikiwa ni pamoja shughuli za uendeshaji kabla ya Mashindano hayo.
No comments :
Post a Comment