LONDON, England
BONDIA Mwingereza Amir Khan anatarajia kurejea ulingoni
Desemba mwaka huu, kupigana na Carlos Molina – huku akiwa chini ya ukufunzi wa
kocha mpya Virgil Hunter anayemnoa kwa sasa.
Khan, 25, analichukulia pambano hilo kama hatua moja mbele
kuelekea mchuano anaouwania wa kupimana ubavu na bondia kama Floyd Mayweather.
Bondia huyo mzaliwa wa jiji la Bolton, hivi karibuni
alimfukuza kazi mkufunzi wake Freddie Roach, kufuatia kichapo kutoka kwa Danny
Garcia Julai mwaka huu, akidai kocha huyo hakuwa na muda wa kutosha kumnoa,
kutokana na majukumu mengine.
Mkali huyu kwa sasa yuko kwenye mazoezi makali chini Hunter nje
ya ‘gym’ yake huko Hayward, California, tayari kumvaa Molina.
Khan alisema: “Kusema kweli nimeridhishwa mno Virgil kuwa
mkufunzi wangu mpya. Kila mmoja miongoni mwa mabondia wanatambua uzoefu, ufundi
na mafanikio ya Virgil aliyopata miaka michache iliyopita.
No comments :
Post a Comment