Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, October 7, 2012

BAADAYE YA OMMY DIMPOZ KUBEBA NYIMBO NANE




Na Elizabeth John
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ anajipanga kuachia albamu yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la ‘Baadae’ ambayo itakua na jumla ya nyimbo nane.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Dimpoz alisema ameamua kuipa albamu yake jina hilo kutokana na kuona wimbo wake wa ‘Baadae’ umefanya vizuri zaidi kuliko ule wa ‘Nai nai’ ambao amemshirikisha nyota wa muziki huo, Alikiba.
“Kiukweli wimbo wa Baadae umefanya vizuri zaidi pamoja na kwamba Nai nai ndio ulinitambulisha katika tasnia hiyo, hivyo nimeamua kuiita albamu yangu jina hilo nikiwa naamini mashabiki wangu wataipenda zaidi,” alisema ommy.
Alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa albau hiyo ambayo anatarajia kuiingiza sokoni mwanzoni mwa mwezi ujao, anawaomba mashabiki wake wakae mkao wa kula kuipokea kazi hiyo.
Kabla ya kutamba na wimbo wake wa ‘Baadae’, Ommy alishawahi tamba na wimbo wake wa ‘Nai nai’ ambao ulimtambulisha vema na kumfanya achukue tuzo mbili ambazo ni wimbo bora wa kushirikiana na msanii bora anayechipukia kwenye Kilimanjaro Music Awards mwaka huu.

No comments :

Post a Comment