Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, October 2, 2012

Tanesco waendelea kukamata wezi wa umeme.



Mafundi na wakaguzi wa mita za shirika la umeme Tanesco Mkoa wa shirika hilo Temeke,  wakikagua moja ya nyumba za eneo la Mtoni Relini Temeke baada ya nyumba hiyo kukutwa na mita mbili huku moja ikiwa haitumiki na hata inayotumika imekutwa ikiwa imeunganishwa umeme kabla haujafika kwenye mita hiyo na kusomwa.
Fundi akionyesha waya zilizounganishwa kuiba umeme kabla hazijafika kwenye mita.
Mkaguzi wa mita wa Shirika la Tanesco Mkoa wa shirika hilo Temeke Abrahamu Kalimile akimuonyesha mteja namna walivyoharibu mita ili waibe umeme mara baada ya kupima pamoja na  kuifungua na kugundua tatizo hilo.
 
 
KAZI ya ukaguzi wa mita za umeme kwa wateja wa Shirika La umeme Tanzania Tanesco Mkoa wa Shirika hilo Temeke iliendelea tena jana na kuwakatia umeme watu watano baada ya kukuta na makosa mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya operesheni ya ukaguzi wa mita hizo uliofanyika jana Mtoni Kwa Azizi Ally eneo la Relini msimamizi wa zoezi hilo Johari Nasibu, alisema jumla ya nyumba 80 walizifanyia ukaguzi.
“Kama tunavyofanya siku zote kwenye zoezi hili leo hii tumefanya hapa mtoni eneo la relini tumefanikiwa kukuta mita nane zikiwa na makosa mbalimbali na hatua za haraka tulizo zichukua ni kuwasitishia huduma kwanza kabla ya kufanya tathmini ya hasara tuliyopata ili waweze kutulipa na kama hawajalipa tunawafikisha mahakamani” alisema Nasibu.
Akifafanua zaidi makosa waliyowakutanayo wateja hao aliyataja kuwa ni pamoja na Wizi kwa njia ya kuharibu mita wateja watano, Kuiba umeme kabla haujafika kwenye mteja mmoja na Kujiunganishia umeme bila ya kufuata taratibu wateja wawili.
Aidha Johari alisema kiasi kikubwa cha umeme kimeibwa na shirika lazima litawachukulia hatua kali za kisheria endapo hawatakubali kulipia umeme walioutumia kwa kipindi chote.

No comments :

Post a Comment