Chumba
cha chini ya Bahari kikionekana kwa mbali kikiendelea na matengenezo
kwenye Hoteli ya Manta Resort Makangale iliyoko Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi, akishusha Nanga
kuashiria kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa chumba cha chini ya bahari
katika Hotelai ya Manta Resort, iliyoko Makangale Kaskazini mwa Kisiwa
cha Pemba jana.
Meneja
wa Hoteli ya Manta Resort Makangale mkoa wa kaskazini Pemba Bwana
Metthew Saus {maarufu kama Babu kwanini) na msaidizi wake wakiwa
tayari kumsubiri mgeni rasmi Balozi Seif Ali Iddi kuweka jiwe la Msingi
na Nanga katika ujenzi wa chumba cha chini ya bahari.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa
na Mkewe Mama Pili Seif Iddi, wakiwa kwenye Boti kuelekea kwenye
uwekaji wa jiwe la msingi na nanga ya ujenzi wa chumba cha chini ya
bahari katika Hoteli ya Manta Resort iliyoko Makangale Mkoa Kaskazini
Pemba.
Mke
wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Pili Seif Iddi akijigeza
moja ya kanzu zilizotengenezwa na wajasiri amali wa Jimbo la Gando
ambayo aliondoka nayo kwa manunuzi.
Balozi
Seif akiwa na Mkewe Mama Pili Seif Iddi wakifuaria bidhaa
zilizotengenezwa wajasiri amali wa Jimbo la Gando huku wakipata maelezo
kutoka kwa mjasiri amali wa kikundi hicho Bibi Faida Hamad Juma.
Wajasiri
amali hao walipata futrsa ya kutangaza bidhaa zao katika hafla ya
uwekaji wa jiwe la nanga la ujenzi wa chumba cha chini ya bahari hapo
Manta Resort Makangale Kaskanzini mwa kisiwa cha Pemba. Picha na Hassan Issa wa – OMPR- ZNZ.
**********************************
Harakati
za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha Sekta ya Utalii
zimeanza kuonyesha dalili za mafanikio kufuatia uwekezaji wa daraja la
juu katika sekta hiyo kuanza kushamiri kidogo kidogo hapa Nchini.
Ujenzi
wa chumba cha chini ya bahari { under water room} ulioanzishwa kama
mradi maalum wa kuvutia watalii wa daraja la kwanza unaofanywa na
Uongozi wa Hoteli ya Manta Resort iliyopo Makangale Mkoa wa Kaskazini
Pemba ni miongoni mwa dalili hizo.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikuwa mgeni rasmi
katika uwekaji wa jiwe la nanga la ujenzi wa chumba hicho kitakachokuwa
chini ya Bahari ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya kutimia miaka
49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Balozi
Seif akiambatana na Viongozi mbali mbali wa Serikali, Wizaraya ya
Habari wakiwemo maafisa wa sekta ya Utalii na wanasiasa alionekana
kufarajika na mradi huo mpya ndani ya Bara la Afrika na ni wa pili
kufanywa Duniani ukitanguliwa na ule wa Sweden ulioko katika maji ya
ziwa.
Akizungumza
katika hafla hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
alisema ni jambo la kutia moyo kuona Kisiwa cha Pemba hivi sasa kinanza
kupanuka Kiutalii kufuatia kuimarika kwa miundombinu iliyowekwa.
Aliwataka
wananchi wa Kisiwa cha Pemba kuchangamkia sera ya Utalii kwa wote kwa
lengo la kuitumia fursa hiyo adhimu kabla haijavamiwa na wafanyakazi wa
nje ya Visiwa hivi.
‘’
Pemba sasa ni eneo ambalo Serikali inaliangalia katika kufunguka
kiutalii hasa kutokana na kukamilika kwa miundombinu ya umeme na Bara
bara’’. Alifafanua Balozi Seif.
Alikumbusha
kwamba Zanzibar bado haijatangazwa kiutalii nje ya Nchi na watu
wanaofikia hatua za kufanya hivyo huitangazia kwa maslahi yao binafsi.
Balozi
Seif ameiagiza Taasisi inayosimamia uwekezaji vitega uchumi Zanzibar {
ZIPA } kuziangalia upya sheria zilizopo za uwekezaji ili kuwepuka
kurejea makosa yaliyojitokeza tokea kuimarishwa kwa sekta ya Utalii
Nchini.
Alisema
ipo miradi ya uwekezaji ambayo imekuwa mtihani kwa serikali kwa vile
imeshindwa kutoa huduma zilizokusudiwa akiutolea mfano mradi wa Hoteli
ya Mawimbini ambao kmwa sasa umeshindwa kufanya kazi.
Akimkaribisha
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Waziri wa Habari,
Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk alisema mradi huo wa
chumba cha chini ya Bahari masafa ya Mita 100 ni wa majaribio.
Mh. Said alieleza kuwa mradi huo wa chumba kimoja utakapofaulu Uongozi wa Hoteli ya Manta Resort umekusudia kujenga vyumba vingi zaidi ili kufanikisha utali wa daraja la juu.
Mapema
Meneja wa Hoteli ya Manta Resort Makangale Bwana Metthew Saus Maarufu
kwa jina la Babu kwa nini alisema wazo la ujenzi wa mradi huu
lilichukuwa takriban miaka saba kwa kufanywa utafiti chini ya bahari.
Babu
kwani alisema Kisiwa cha Pemba kina mazingira mazuri ya kuendeleza
mradi huo ikilinganishwa na mradi wa mwanzo Duniani kama huo
ulioanzishwa Nchini Sweden.
Amewapongeza
wananchi wa Zanzibar kwa kusherehekea miaka 49 ya mapinduzi Matukufu ya
mwaka 1964 yaliyowatoa katika makucha ya wakoloni.
Mradi
huo wa chumba cha chini ya Bahari unaokisiwa kugharimu Dola za
Kimarekani Laki Tano sawa na Shilingi za Kitanzania Milioni Mia
758,000,000/- utakamilika rasmi ndani ya muda wa siku Tisini.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
No comments :
Post a Comment