Abiria
wa kike mwenye asili ya kigeni 'Mzungu', akimsaidia dereva wake wa
Bajaji, ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, baada ya
usafiri wao wa Bajaji kupata pancha eneo la Lugalo Jeshini Barabara ya
Bagamoyo, jijini Dar es Salaam, leo asubuhi. Abiria huyo mwanamama
alionyesha ushirikiano wa hali ya juu huku akimsaidia dereve huyo kuinua
Bajaji hiyo upande mmoja ili waweze kufungua tairi bovu na kubadili na
kuendelea na safari yao na kuwaacha hoi watu wote waliokuwa wakiwaona
katika harakati zao. Je angekuwa ni abiria mwanamke wa 'Kibongo'
angeweza kutoa msaada huu wa hali na mali kwa kumsaidia dereva wake au
ndo kwanza angesimamisha Bajaji nyingine na kusepa zake???
''Hadi kieleweke'' Abiria mzungu, akimsaidia dereva wakekuinua Bajaji ili kubadili tairi.....
''Moja, Mbili, Tatuuuu, Haya twendee........Imeinuka kazi sasa kufungua tairi.
Shuguli ilianza hivi Mdada mzungu akiwa na vijitambaa mkononi kwa ajili ya kushikia bodi la Bajaji kuepuka kuumia mikono.
No comments :
Post a Comment