Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameita kambini wachezaji 24 kujiandaa
kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa
Septemba 7 mwaka huu nchini humo.
Wachezaji
hao wanatakiwa kuripoti kambini Agosti 29 mwaka huu kabla ya saa 1
kamili usiku. Kambi ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium
Lager itakuwa kwenye hoteli ya Accommondia jijini Dar es Salaam.
Makipa
walioitwa katika timu hiyo Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam),
Ally Mustafa (Yanga) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris
(Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Nadir Haroub
(Yanga), Erasto Nyoni (Azam), Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar) na David
Luhende (Yanga).
Viungo
Khamis Mcha (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Dilunga (Ruvu
Shooting), Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd (Yanga), Haruna Chanongo
(Simba), Amir Kiemba (Simba), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon Msuva (Yanga),
John Boko (Azam), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi
ya Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo)
na Juma Liuzio (Mtibwa Sugar).
RAMBIRAMBI MSIBA WA BARAKA KITENGE
Shrikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha
mchezaji wa zamani wa timu za Yanga na Taifa Stars, Baraka Kitenge (74)
kilichotokea leo mchana (Agosti 20 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Msiba
huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti
Kitenge akiwa mchezaji, alitoa mchango mkubwa kwa timu mbalimbali
alizochezea, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
Kitenge
amefia Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo alikuwa amelazwa
akisumbuliwa na kansa ya uti wa mgongo. Enzi zake katika Yanga na Taifa
Stas alicheza na wachezaji kama akina Athuman Kilambo na Abdulrahman
Juma.
TFF
inatoa pole kwa familia ya marehemu Kitenge, Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na klabu ya Yanga na kuwataka kuwa na
subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Mipango
ya mazishi inafanywa nyumbani kwa Marehemu, Yombo Vituka (Jet) jijini
Dar es Salaam. Mungu aiweke roho ya marehemu Kitenge mahali pema peponi.
Amina
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments :
Post a Comment