Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, August 27, 2013

Chadema yaanza kumliza Nkamia, yashinda uchaguzi jimboni kwake



 Kaimu Katibu wa Chadema Wilaya ya Dodoma Mjini, Jella Kheri Mambo, akiwa Ofisini kwake.
Ofisi ya Chadema Wilaya ya Dodoma Mjini

Na Bryceson Mathias, Kondoa

KATIKA hali inayoonesha ni kumliza Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kijiji cha Mlongila Kata ya Jangalu, Jimbo la Kondoa Kusini, Kimeshinda kwa kishindo uchaguzi wa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho.

Hatua ya Chadema kuonesha kinakubalika hadi vijijini, kilishinda uchaguzi huo uliofanyika Jumamosi, Agosti 24, ambapo Mgombea wa Chadema, Sariah Bakari Lubuva Alishinda kwa kura 184 na kuwatupa mbali wagombea wenzake baada Mwenyekiti aliyekuwepo kujiuzulu.

Akizumza na Mwandishi wa habari hizi Katibu Mkuu wa Chadema mkoani Dodoma, Stephen Masawe, alithibitisha mgombea wao Lubuva kushinda kwa kura (184), dhidi ya kura za Chama cha Mapinduzi (CCM) waliopata (96) na Chama cha wananchi (CUF) waliopata (9).

“Hizo ni salamu na Mvua za rasharasha kwa Nkamia anayedai anapenda kuzungumza na mwenye Mbwa badala ya Mbwa, lakini Chadema tunazungumza na Nguvu ya Umma yenye Hati Milki ya Tanzania”.alisema Masawe.

Wakati huo huo Kaimu Katibu wa Wilaya ya Dodoma Mjini (Chadema), Jella Kheri Mambo, amekanusha Kauli ya Viongozi wa CCM Mkoa wa Dodoma wanaomtuhumu kuwa yeye na wenzake waliojiunga Chadema wako huko kwa Mkopo.

Alisema Kauli ya viongozi wa CCM Mkoa ni ya Fisi aliyenyatia mkono wa mtu akidhani utaanguka, lakini hadi safari inakwisha haukuangua naye akaambulia Patupu asiupate.

“Nilikataa zawadi ya uongo wa Ufisadi wa Makusanyo ya Mil.1,5/= badala ya Sh. Mil.5/- zilizostahili kukusanywa kwa nyumba 500 za Kata ya Uhuru kila nyumba 10,000/-. Viongozi hao wakafanya njama kuniondoa, hivyo siwezi kurudi CCM“.alisema Mambo.

Aidha badala yake Mambo amesema, hivi karibuni Chadema Dodoma Mjini kinaanza kampeni maalum (M4C) ya Mlango kwa Mlango kuzungukia Kata 37 wilayani humo,ili kuongeza Idadi ya wanachama wake, mbali ya wale inaowapata kwenye Mikutano ya hadhara kila mara.

Nilikuwa mmuumini wa Azimio la Arusha na sera za Chadema ni hizo ambazo mimi ni muumini wake. Wananchi na Viongozi wapuuzeni CCM walioshindwa kuwatetea wananchi badla yake wanawafanya watumwa wa kuwasomeshea, kuwalisha na kuwavisha watoto wao”.alisema Mambo.

No comments :

Post a Comment