Mshambuliaji
wa Yanga, Didier Kavumbagu (wa pili kushoto) akiwania mpira na mabeki
wa Ashanti, wakati wa mchezo wa fungua dimba la Ligi Kuu ya Vodacom,
Tanzania bara uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es
Salaam. Katika mchezo huo Yanga imechabanga Ashanti jumla ya mabao 5-1.
Bao
la kwanza lilifungwa na Jerson Tegete, katika dakika ya 10, bao la pili
likafungwa na Simon Msuva, katika dakika ya 47, na la tatu likafungwa
tena na Jerson Tegete, katika dakika ya 57, la nne likawekwa kimiani na
Haruna Niyonzima katika dakika ya 73 na lakufunga pazia hilo la mabao ya
Yanga, liliwekwa Kambani na Nizar Khalfan, katika dakika ya
90+aliyetokea Benchi akichukua nafasi ya Jerry Tegete.
Ni Juma Abdul Katikati ya mabeki wa Ashanti.
Niyonzima akichanja mbuga.
Sehemu ya mashabiki wa Ashanti
Sehemu ya Mashabiki wa Ashanti.
Hivi ndivyo, Haruna Niyonzima alivyowakalisha mabeki wa Ashanti na kukosa bao la wazi katika kipindi cha kwanza.
Mabeki wa Ashanti, walikaa.......
YANGA ilianza na :-
Ali Mustafa 'Bartez', Juma Abdul, David Luhende, Nadir Haroub
'Canavaro', (c) Mbuyu Twite, Athuman Idd, 'Chuji', Simon Msuva, Salum
Telela, Didier Kavumbagu, Jerson Tegete na Haruna Niyonzima.
BENCHI LA AKIBA:-
Deogratias Munishi, Oscar Joshua, Frank Domayo, Bakari Masoud, Nizar Khalfan, Issa Ngao na Husein Javu.
ASHANTI ilianza na:-
Ibrahim
Abdallah, Khan Usimba (c), Emaanuel Kichiba, Ramadhan Malima, Tumba
Sued, Emmanuel Memba, Fakihi Hakika, Mussa Nampaka, Hussein Sued, Mussa
Kanyaga na Joseph Mahundi.
BENCHI LA AKIBA:-
Daud Mwasongwe, Hussein Mkongo, Paulo Telly, Mwinyi Abdulrahim, Laurent Mugia, Peter Ilunda na Shaban Juma.
HUKO KWINGINEKO:
Coastal Union, wameichapa JKT Oljolo 2-0 katika uwanja wa Sheikh Amri
Abeid jijini Arusha, Mtibwa na Azam Fc, wametoshana nguvu kwa kufungana
1-1, katika Uwanja wa Manungu Morogoro, Mbeya City na Kagera Sugar
wametoka suluhu 0-0, katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya. Huko mkoani
Tabora Simba imetoka sare ya 2-2 na Rhyno, katika Uwanja wa Ali Hassan
Mwinyi, JKT Ruvu imewafunga Mgambo JKT 2-0.
No comments :
Post a Comment