Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, August 25, 2013

MWENYEKITI WA CCM JK AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU DODODMA


 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao maalum cha Kamati Kuu ya CCM, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma leo, Agosti 25, 2013. Kikao hicho kilifanyika kwa ajili ya kukutana Mbunge wa Bukoba mjini Khamis Kagasheki, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera, Constansia Buhiye,  Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Abedi Mushi, Mwenyekiti na Katibu wa CCM wilaya ya Bukoba mjini na Meya wa Manispaa ya Bukoba Anatory Amani, kuhusu mgogoro wa madiwani wanane wa CCM Manispaa ya Bukoba. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Constansia Muhiye na Katibu wa CCM wa mkoa huo, Abedi Mushi wakisubiri kuingia ukumbini kukutana na Kamati kuu mjini Dodoma leo.
 Mbunge wa Bukoba mjini Khamis Kagasheki akisubiri kuingia ukumbini kukutana na Kamati Kuu ya CCM Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akimsikiliza kwa makini Mwana-CCM mwenye ulemavu wa miguu, Shija Luhende kutoka Mwanza, ambaye alimkuta kwenye viwanja vya Makao Mkuu ya CCM mjini Dodoma leo, akitafuta msaada wa baiskeli. 
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,  Abdallah Bulembo akizungumza na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Jenista Mhagama, nje ya ukumbi, Makao Mkuu ya CCM mjini Dodoma, leo. Picha na Bashir Nkoromo

No comments :

Post a Comment