Mkuu
wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw.Peter
Ngota akikabidhi msaada wa vyakula kwa Mwenyekiti wa Shirika la Femele
Youth Help Age Trust,Bw Simon Mganga lililoko Pangani-Kibaha
linalohudumia watoto yatima,na wanaoishi katika mazingira magumu katika
hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam jana kusherehekea sikukuu ya
Eid.
Mkuu
wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Mawasiliano Tanzania, Bw.Peter Ngota
akikabidhi msaada wa vyakula kwa wawakilishi wa shirika la Missionary of
Charity la watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu katika
hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam jana kusherehekea sikukuu ya
Eid.
Na mwandishi wetu, Dar es salaam
Wadau
wa maendeleo wametakiwa kuendeleza juhudi za kusaidia jamii hasa watu
waishio katika mazingira magumu ili kuleta maendeleo na ustawi katika
jamii.
Wito
huo umetolewa na Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Mawasiliano
Tanzania, Bw.Peter Ngota jijini Dar es salaam jana wakati akikabidhi
msaada wa vyakula kwa vikundi vya watu wenye mahitaji ikiwa ni sehemu ya
kampuni hiyo kushiriki katika kusaidia jamii na kusherehekea sikukuu ya
Eid.
Akizungumza
katika hafla hiyo alisema kuwa kuna umuhimu wa wadau mbalimbali
kushiriki katika kusaidia makundi ya watu wenye mahitaji ili nao waweze
kupata huduma za msingi ikwemo elimu, afya na chakula.
Amesema
kuwa TTCL inatambua uwepo wa makundi hayo ndio maana imeamua kuungana
nao hasa wakati huu wa sikukuu ya eid el fitri ili nao watambue kuwa
wanathaminiwa kama sehemu ya jamii.
Bw.
Ngota amesema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikishiriki katika shughuli za
kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kusaidia jamii katika sekta mbalimbali.
Kwa
upande mwingine, aliwaasa watoto wanaosaidiwa na vituo hivyo kujitahidi
katika masomo na kufanya vizuri ili waje kufanya kazi katika kampuni
hiyo ya wazawa hapa nchini.
“Nawaasa
mjitahidi katika masomo ili hapo baadaye mje kufanya kazi katika
kampuni hii,” alisema. Akizungumza kwa niaba ya watoto wanaoishi katika
mazingira magumu,mtoto Emiliam Joseph ameishukuru kampuni hiyo kwa
msaada huo na kuomba wadau wengine kuendeleza juhudi hizo.
Mwenyekiti
wa shirika linalohudumia watoto yatima na wanaoishi katika mazigira
magumu,Femele Youth Help Age Trust, Bw. Simon Mganga ameishukuru kampuni
hiyo kwa msaada huo na kukiri kuwa kampuni hiyo imekuwa mmoja wa wadau
muhimu katika kusaidi shirika lake.
Naye
mwakilishi wa shirika la Missionary of Charity, St Mary Domitila
amesemakuwa msaada waliopata una thamani kubwa kwao kwani itoaji wa
msaada huwa hauangalii kiasi bali ni nia ya dhati ya mtu kuamua kusaidia
na hivyo kutoa wito kwa wadau wengine keundelea kusaidia.
Msaada huo wenye jumla ya Tsh milioni tatu unajumuisha mchele,unga wa mahindi,mafuta ya kupikia na majani ya chai.
Pia TTCL ilitoa simu kwa mashirika hayo katika juhudi za kuwarahisishia mawasiliano.
Pia TTCL ilitoa simu kwa mashirika hayo katika juhudi za kuwarahisishia mawasiliano.
Kwa muda mrefu sasa, TTCL imekuwa ikishiriki kutoa msaada kwa vituo vinavyohudumia watu wanaoishi katika mazingira magumu.
No comments :
Post a Comment