BAADA ya kushindwa kuitambulisha mara kadhaa ngoma yake mpya inayofahamika kwa jina la ‘Topogo’, mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, ameisambaza ngoma hiyo katika vituo mbalimbali vya redio.
Dimpoz
amehairisha utambulisho wa ngoma hiyo zaidi ya mara moja ambapo mara ya
mwisho alitakiwa kuitambulisha katika ukumbi wa Kimataifa Club
Bilicanas, Juni 30 kabla hajausambaza wiki iliyopita.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Ommy Dimpoz alisema ameamua kuusambaza wimbo
huo bila kuutambulisha kutokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wake
na anawaomba wapenzi wa kazi zake waupokee wimbo huo kwa mikoni miwili.
Alisema
katika wimbo huo, kamshirikisha nyota kutoka Nigeria, J Martin na
kwamba anaamini kutakuwa na changamoto nyingi kwa wasanii wa bongo
kutokana na uwepo wa mkali huyo.
“Kiukweli
J Martin ni msanii mkubwa na ana uwezo wa kulitawala jukwaa anapokuwa
kazini; naamini nitafanya vizuri zaidi, ndiyo maana nimeamua
kushirikiana naye, cha muhimu ni sapoti katika kazi zangu,” alisema
Dimpoz.
Licha
ya kutoka na nyota huyo, Dimpoz kwa sasa anatamba na kibao chake cha
‘Me and You’ alichomshirikisha chipukizi wa muziki huo, Vanesa Mdee,
mbali na kuwa na vibao vingi ambavyo vimefanya vizuri katika tasnia ya
muziki wa bongo fleva.
No comments :
Post a Comment